Monday, December 3, 2018

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWATAKA WAAJIRI NCHINI KUWAPATIA HUDUMA STAHIKI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU ILI WAWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU



    Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akifungua kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bi Agnes Meena, Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008  ili aweze kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mwongozo huo katika taasisi za umma nchini.

Afisa Tawala Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi,  Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi baada ya kufunga kikao kazi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment