Tuesday, February 23, 2021

NDEJEMBI AHIMIZA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA

James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Tarehe 23 Februari, 2021

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewahiza Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha huduma zitolewazo na Wakala hiyo.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala hiyo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kujitambulisha, kufahamu kwa kina makujumu ya Wakala hiyo, kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watumishi wa Wakala hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Ndejembi amewapongeza Watumishi wa Wakala hiyo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na weledi kwani hakuna maafa yoyote yaliyowahi kujitokeza tangu Serikali ianze kumiliki ndege zake. 

Mhe. Ndejembi amesema, Wakala hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha matengenezo ya ndege yanafanyika kwa wakati ili ziendelee kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa Mhe. Rais na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za Viongozi hao wa Kitaifa zinatekelezwa kama zilivyopangwa.

Aidha, Mhe. Ndejembi ameahidi kuzifanyia kazi changamoto za Wakala hiyo ili kuwawezesha Watumishi wa Wakala hiyo kuwa na mazingira bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Ndejembi amewaasa watumishi hao kuendelea kuchapa kazi wakati changamoto zao zikifanyiwa kazi.

Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa tarehe 17 Mei, 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Wakala ya Ndege za Serikali Na.3 ya Mwaka 1997 kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha usalama wa usafiri wa ndege kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wanaotumia ndege hizo. Pamoja na jukumu hilo, Wakala ina jukumu la kuratibu kwa niaba ya Serikali ununuzi wa ndege mpya za biashara, kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kusimamia mikataba ya ukodishwaji wa ndege hizo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.



Mtumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Salahe Harun Mwanauta ambaye ni Rubani akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Mtumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Bernard Joseph Mayila akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) Dkt. Benjamin Ndimila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.



Thursday, February 18, 2021

NDEJEMBI AKEMEA WAAJIRI WANAOWABADILISHIA VYEO VYA KIMUUNDO KINYUME NA TARATIBU MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI KATA WALIOAJIRIWA MWAKA 2018

 Na. James K. Mwanamyoto-Iringa

Tarehe 18 Februari, 2021

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Waajiri kutowabadilishia vyeo vya kimuundo Maafisa Tarafa na Watendaji Kata walioajiriwa mwaka 2018 wakiwa na taaluma mbalimbali kwa lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliostaafu na walioondolewa baada ya kubainika kuwa na vyeti vya kughushi.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo Mkoani Iringa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali mkoani humo.

Mhe. Ndejembi amesema, wapo baadhi ya Waajiri wamewabadilishia watumishi hao vyeo vya kimuundo bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye mwenye mamlaka ikizingatiwa kuwa alishatoa maelekezo ya kutowabadilishia kada wala kuwahamisha vituo vya kazi mpaka watakapotimiza miaka mitano.

"Watumishi hao wakati wa kuajiriwa, walisaini mikataba ya kutumikia vyeo vyao bila kubadilisha wala kuhama mpaka watakapotimiza miaka mitano, hivyo Waajiri kama mna upungufu wa Watumishi ambao wana sifa walizonazo watumishi hao, muombe kibali kwa Katibu Mkuu Utumishi ili mpatiwe watumishi mbadala." Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema changamoto ya Watumishi wa Umma kukaimu nafasi za uongozi kwa muda mrefu inatokana na baadhi ya waajiri kuwakaimisha Watumishi nafasi mbalimbali bila kuwa na kibali cha Katibu Mkuu Utumishi. 

Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, asilimia zaidi ya 60 ya wanaokaimu hawana sifa za kutumikia vyeo walivyokaimishwa, hivyo wanapoteza sifa za kupata kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na stahiki husika.

Ametoa wito kwa Waajiri kuwaombea vibali kwa wakati kwa Katibu Mkuu Utumishi watumishi ambao wana sifa za kukaimu ili waweze kupata uhalali wa kutumikia vyeo walivyokasimiwa na kupata stahiki husika na kuongeza kuwa, hivi sasa ofisi yake inatoa vibali vya kukaimu kwa wakati ndani ya wiki tatu.

Mhe. Ndejembi amefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma zilizopo mkoani humo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani Iringa kwenye Ukumbi wa Manispaa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi hao.


Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao kwenye Ukumbi wa Manispaa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi hao.

 



Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda akiwasilisha changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi mkoani Iringa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu hoja za kiutumishi zilizowasilishwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Iringa yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.

 

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.



Wednesday, February 17, 2021

NDEJEMBI ATAKA KILA MTUMISHI WA UMMA KUWA NA MPANGO KAZI ILI KUONDOKANA NA UFANYAJI KAZI WA MAZOEA

James K. Mwanamyoto-Mpwapwa

Tarehe 17 Februari, 2021

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka kila Mtumishi wa Umma nchini kuwa na mpango kazi utakaomuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa umma.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma.

Mhe. Ndejembi amesema, ni jukumu la Waajiri kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza mpango kazi wake ili kutoa mchango wa kiutendaji mahala pa kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo halina tija katika maendeleo ya taifa.

Sanjali na hayo, Mhe. Ndejembi amewasisitiza Watumishi wa Umma kuzingatia ujazaji wa fomu za Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) ili kutoa fursa kwa Waajiri kupima utendaji kazi wa watumishi wao kwa lengo la kuwapa stahiki kulingana na utendaji kazi wao.

“OPRAS ipo kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2008 pamoja na Sheria ya Utumishi Sura Namba 298, hivyo ni jukumu la waajiri kuhakikisha watumishi wanajaza fomu na kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wao ili kuongeza ufanisi kiutendaji.” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Akijibu hoja ya Bw. Kandindo Mumeli, mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhusu baadhi ya waajiri kutotenga bajeti ya kuwahudumia Watumishi wa Umma wenye Ulemavu kama Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa Mwaka 2008 unavyoelekeza, Mhe. Ndejembi amewataka Waajiri kutoa kipaumbele cha kutenga fedha za kuwahudumia watumishi hao ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesisitiza juu ya usimamizi wa ruzuku inayotolewa na Serikali kwa wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, ambapo amesema, ni jukumu la kila Mtumishi wa Umma kuhakikisha fedha wanazopokea wanufaika wa TASAF zinatumika kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Kumekuwa na mtazamo hasi juu ya usimamizi wa fedha za TASAF kuwa ni jukumu la Waratibu wa TASAF pekee, jambo ambalo halina tija kwa taifa kwani usimamizi wa fedha za umma ni jukumu la kila mtumishi, hivyo ni wajibu wetu sote kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.” Mhe. Ndejembi ameongeza.

Pia, Mhe. Ndejembi amepiga marufuku kitendo cha kukata fedha za wanufaika wa TASAF ili kuchangia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwani kitendo hicho kinawakwamisha wanufaika kutumia ruzuku waliyopewa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazoboresha maisha yao.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, wanufaika wa TASAF waachwe huru kutumia ruzuku wanazopatiwa katika shughuli mbalimbaliz za maendeleo ili watakachozalisha ndio wakitumie kuchangia CHF kwa hiari.

Lengo la ziara ya Mhe. Ndejembi katika Wilaya hizo ilikuwa ni kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.


Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.



Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Kandido Mumeli Akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu hoja ya Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Kandido Mumeli aliyoiwasilisha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi Wilayani Kongwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi Wilayani Kongwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.


Monday, February 8, 2021

WATUMISHI TULINDE AFYA ZETU ILI TUWAHUDUMIE WANANCHI IPASAVYO - Dkt. Ndumbaro

 Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma.

Tarehe 08 Februari, 2021 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amewataka Watumishi wa Umma nchini kulinda afya zao ili waweze kuwahudumia vema wananchi wanaofuata huduma mbalimbali katika taasisi zao.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo mapema leo wakati akizungumza na Watumishi wa ofisi yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Dkt. Ndumbaro amesema, ili Watumishi wa Umma waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hawana budi kulinda afya zao ikizingatiwa kuwa  wakati wa utoaji huduma wanakutana na watu ambao baadhi yao wanaweza kuwa na changamoto mbalimbali za kiafya.

Ili kuhakikisha taifa linakuwa na rasilimaliwatu yenye tija, Dkt. Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara na kupata tiba mapema iwezekanavyo pindi wanapohisi kukabiliwa na changamoto yoyote ya kiafya.

Sanjali na hilo, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi wa Umma kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya kwa lengo la kuendelea kutoa mchango katika ujenzi wa taifa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amekuwa na utaratibu wa kukutana na Watumishi wa Umma katika maeneo mbalimbali nchini kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma alipokutana nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.