Wednesday, December 31, 2014

Monday, December 15, 2014

WATAALAMU 12 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPANI WAMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mtalaamu wa kujitolea Bw.Keisuke Yamamoto akitoa mada wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka Japani iliyofanyika Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.Mick Kiliba (kushoto) akimpongeza mmoja kati ya watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Keisuke Yamamoto baada ya kumaliza muda wa kujitolea nchini.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. Mick Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini mara baada ya hafla fupi iliyofanyika Utumishi.Wengine ni Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Thursday, December 11, 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Maadili ya Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. Mathew Kirama akitoa maoni katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya maadili katika Utumishi wa Umma.

Mtaalamu mwelekezi toka Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Francis Mwaijande (wa pili toka kushoto) akiwasilisha matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA Bw. Joseph Mbando (aliyesimama) akitoa maoni katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji maadili katika Utumishi wa Umma.

Monday, November 17, 2014

UBALOZI WA INDIA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MPANGO WA USHIRIKIANO WA KIUFUNDI NA UCHUMI WA SERIKALI YA INDIA (ITEC)




Baadhi ya wageni waalikwa na wanufaika wa Mpango wa Mafunzo Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi wa Serikali ya India (ITEC)  wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mpango huo yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India jijini Dar es Salaam.

Balozi wa India nchini Tanzania Mh.Debnath Shaw akizungumza wakati wa sherehe za  maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Mafunzo Ushirikiano wa Kiufundi na Kiuchumi wa Serikali ya India (ITEC)  yalichofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India jijini Dar es Salaam.


 Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto),Balozi wa India nchini Tanzania Mh.Debnath Shaw (wa pili kutoka kushoto)  na wageni waalikwa wakiangalia filamu ya mpango wa mafunzo ya India wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi na Uchumi wa Serikali ya India (50 YEARS ITEC DAY) yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India  jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mpango wa Ushirikiano wa Kiufundi na Uchumi wa Serikali ya India (50 YEARS ITEC DAY) yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni wa India  jijini Dar es Salaam


Thursday, October 23, 2014

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA,DODOMA NA TUME YA MIPANGO

Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

Afisa Utumishi Mwandamizi  wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  wakifuatilia mada.


Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Kielektroniki (video conference) kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo 

Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakifuatilia mada  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.


Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Magreth Ngondya (kushoto) akiwasilisha mada katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia Ki- elektroniki (video conference) katika kikao kazi kati ya Utumishi  na Mikoa ya Singida, Arusha,  Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.

Friday, October 17, 2014

KLABU YA MICHEZO YA UTUMISHI YAKABIDHI VIKOMBE KWA WAZIRI KOMBANI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuzipongeza timu zilizoshinda mashindano ya SHIMIWI yaliyomalizika mjini Morogoro hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo wa Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) (katikati) kuzungumza na watumishi katika hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda kwa kishindo katika Michezo ya SHIMIWI 2014.Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.
Baadhi ya watumishi  wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda michezo ya SHIMIWI katika ukumbi wa Utumishi.
Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Utumishi  Bw.Hassan Ligoneko akimkabidhi kombe Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akitoa mkono wa pongezi kwa Timu ya mpira wa pete ya Utumishi katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake.

Wednesday, October 15, 2014

UTUMISHI BINGWA MPYA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi Bw. HAB Mkwizu akimkabidhi kapteni wa Utumishi Bi. Elizabeth Fusi kombe la mshindi wa kwanza mpira wa pete siku ya kilele cha mashindano ya SHIMIWI 2014 uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera na viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi Bw. HAB Mkwizu akimkabidhi kombe mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Utumishi Bw. Hassan Ligoneko (kulia) siku ya kilele cha mashindano ya SHIMIWI 2014 uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Wachezaji wa Ofisi ya Rais Utumishi wakiwa katika maandamano huku wakipunga mkono kwa mgeni rasmi siku ya kilele cha mashindano ya SHIMIWI 2014 uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa kwa Mashindano ya 38 ya SHIMIWI kwa mwaka 2014.
Utumishi imefanikiwa kuwa bingwa baada ya kuisambaratisha timu Wizara ya Afya kwa ushindi mnono wa Pete 65 kwa 35 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Katika mchezo huo, wachezaji Fatuma Machenga (GS) na Anna Msulwa (GA) wa Utumishi wakicheza kwa ushirikiano waliliongoza jahazi la Utumishi na kufanikisha ushindi huo mnono. Machenga (GS) alifanikiwa kufunga 45 na Msulwa (GA) 20 hivyo kuhakikisha Utumishi inakua bingwa.
Mara baada ya mchezo kumalizika, kocha wa timu ya Afya Mwajuma Kisengo alisema mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani ila bahati haikua yao na wanasubiri mashindano yajayo.
“Mimi kama kocha na mwamuzi wa kimataifa nawapongeza wachezaji wangu na wenzao wa Utumishi, pamoja na waamuzi ambao wamechezesha vizuri kwa kuzingatia sheria za mchezo huu” Kisengo alisema.
Naye kocha wa Utumishi Bw. Methew Kambona aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kunyakua kombe la SHIMIWI 2014.
Utumishi ilifuzu hatua ya fainali baada ya kuifungashia virago Ikulu ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa jumla ya magoli 42 dhidi ya 41 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Saturday, October 11, 2014

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NDIO MABINGWA WA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014


Mabingwa wapya wa SHIMIWI 2014, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Afya na kunyakua kombe la SHIMIWI 2014 mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Hekaheka ya kuwania mpira baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) na Afya katika mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Afya aliyeruka juu akifanya jitihada za kuuzuia mpira ulioelekezwa golini  ili usilete madhara wakati wa mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 ulioikutanisha timu yake na Utumishi katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Mashabiki wa timu ya mpira wa pete ya Ofisi ya Rais,Utumishi wakiishangilia timu yao wakati wa fainali iliyoikutanisha timu yao na Afya katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.


Baadhi ya washabiki wa mchezo wa mpira wa pete wakishuhudia fainali kati ya Utumishi na Afya wakati wa mchezo uliozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.