Sunday, May 28, 2023

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEKELEZA MAELEKEZO YA MHE. RAIS YA KUHUISHA MIUNDO YA MAENDELEO YA UTUMISHI YA KADA ZA MAKATIBU MAHSUSI NA WATUNZA KUMBUKUBU NA NYARAKA ITAKAYOANZA KUTUMIKA MWEZI JULAI, 2023

 Na. Veronica E. Mwafisi-Zanzibar

Tarehe 28 Mei, 2023

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imetekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhuisha Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Kada za Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka ambayo itaanza kutumika Julai 1, 2023.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Rais wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar tarehe 27/05/2023.

Mhe. Simbachawene amesema pamoja na maelekezo ya kuhuisha muundo huo, Mhe. Rais pia alielekeza kukiwezesha na kukipa hadhi Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tabora kuzalisha Makatibu Mahususi wenye viwango na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa ambapo Chuo hicho kimeboresha mitaala yake ambayo imeshaidhinishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) ambao utaanza kutumika kuanzia mwaka wa masomo wa 2023/24 unaoanza mwezi Oktoba, 2023.

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa katika kushughulikia uhaba wa watumishi wa kada hizi mbili ndani ya Utumishi wa Umma, Serikali imetoa vibali 512 vya ajira mpya wa kada za Makatibu Mahsusi na nafasi 443 na ajira mpya kwa kada za Watunza Kumbukumbu na Nyaraka katika mwaka wa fedha 2022/23.

Pia, katika mwaka wa fedha 2023/24, Ofisi ya Rais-UTUMISHI imeidhinisha jumla ya nafasi 775 za ajira mpya za kada ya Makatibu Mahsusi na nafasi 930 za ajira mpya za kada za Watunza Kumbukumbu na Nyaraka.

Mhe. Simbachawene amesema kwa kutambua mchango wa kada hizi mbili katika ustawi wa Utumishi wa Umma, jumla ya watumishi 450 wa kada za Makatibu Mahususi wamepandishwa vyeo na kuidhinishiwa mishahara mipya kuanzia mwezi Mei, 2023 na watumishi wengine 462 wanarajiwa kuidhinishiwa vyeo na mishahara mipya mwezi Juni, 2023. Hivyo kufanya idadi ya Watumishi waliopandishwa vyeo kufikia 912.

Aidha, jumla ya Watunza Kumbukumbu 394 waliokasimiwa katika Ikama na Bajeti ya mwaka 2022/23 wameshapandishwa vyeo na kuidhinishiwa mishahara ya vyeo vipya mwezi Mei, 2023 na watumishi wengine 255 wanatarajiwa kuidhinishiwa vyeo na mishahara mipya mwezi Juni, 2023. 

Katika mkutano huo, zaidi ya Wanachama 7,943 wa TAPSEA na TRAMPA walikula kiapo cha uadilifu na Utunzaji wa Siri mbele ya Mhe. Rais kutokana na unyeti na umuhimu wa majukumu wanayoyatekeleza.

Mhe. Simbachawene amemshukuru Mhe. Rais kwa maelekezo yake ya kukutanisha vyama hivi pamoja na kufanyia Mkutano Zanzibar ambapo imeongeza undugu na mshikamano kwa kada hizi mbili na Wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Amemhakikishia kuwa, Serikali zote mbili kupitia Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ya JMT itaendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi wa TRAMPA na TAPSEA, kusimamia utendaji kazi wa Watalaamu wa kada hizi mbili pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kisera, Kitaaluma na kiutendaji ili kuwezesha utoaji wa huduma bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.

Mkutano huo wa pamoja umefanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Vyama hivi viwili kwa lengo la kudumisha mshikamano wa kada hizi mbili kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akitoa maelezo mafupi kwa    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mkutano wa Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.


Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wapili kutoka kushoto) akifurahia jambo kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhitimisha kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa utambulisho wa Viongozi na Watendaji wa Serikali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.

 


Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakila kiapo cha Uadilifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar.

 


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyenyoosha kidole) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Bw, Idrisa Mustafa (wapili kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Bw. Omar Gora (wakwanza kulia) kabla ya kuhitimishwa kwa kilele cha Mafunzo ya Uadilifu kwa Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika Zanzibar. Wakwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi.



 

Friday, May 26, 2023

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YASISITIZA UZINGATIAJI WA MAADILI YA UTENDAJI KWA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA TANZANIA



Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa salamu za Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Sehemu ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakiwa kwenye mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi wakifuatilia mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Bw. Omar Gora wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania, Bi. Devotha George akielezea lengo la mafunzo maalumu kwa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Watendaji wa Taasisi za Serikali wakifuatilia mafunzo maalumu kwa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felister Shuli akiwasilisha mada kuhusu haki na wajibu wa mtumishi wa umma wakati wa mafunzo maalumu kwa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.



Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika akiwasilisha mada kuhusu misingi ya maadili ya utendaji katika utumishi wa umma wakati wa mafunzo maalumu kwa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.


Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akiteta na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete baada ya kuzungumza na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakiwasili kuzungumza na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa mafunzo maalumu kuhusu Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri sehemu za kazi yanayoendelea katika Ukumbi wa Golden Tulip-Zanzibar.

 




Thursday, May 25, 2023

VIONGOZI NA WATENDAJI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAWASILISHA MADA NA KUTOA UFAFANUZI WA MASUALA YA KIUTUMISHI KWENYE MKUTANO WA KUMI WA KITAALUMA WA TAPSEA ULIOANZA JANA MKOA WA KUSINI UNGUJA, ZANZIBAR



Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa salamu za Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 


Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akitoa salamu za Ofisi yake katika mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akifuatilia Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifuatilia Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Bi. Zuhura Maganga akitoa neno la utangulizi kabla ya kuwakaribisha Viongozi kuzungumza na washiriki katika Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 



Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika akifafanua hoja kuhusiana na masuala ya maadili kwenye Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.


Mkurugenzi Msaidizi wa Mishahara, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Gubas Vyagusa akifafanua hoja kuhusiana na masuala ya kiutumishi kwenye Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa kwenye Mkutano wa Kumi wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

 


Friday, May 19, 2023

MHE. SIMBACHAWENE NA MHE. RIDHIWANI WAHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Sehemu ya Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (meza kuu katikati) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watendaji hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Menejimenti ya Tume hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete.


Mtumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Confort Kimaro akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kulia) wakisikiliza hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Tume wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Charles Mulamula (aliyevaa miwani) akieleza majukumu ya kitengo chake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimmiza uwajibikaji.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Cheyo akieleza majukumu ya kitengo chake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachaene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Utumishi wa Umma kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Katibu, Idara ya Ukaguzi na Uzingatiaji wa Masuala ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi (aliyesimama) akitoa neno la shukrani mara baada ya   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuhitimisha kikao kazi chake na Menejimenti ya Tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na Menejimenti ya Tume hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete na kulia kwake ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama.





KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA OFISI YA RAIS-UTUMISHI


 

Wednesday, May 17, 2023

WAAJIRI WATAKIWA KUWARUHUSU MAKATIBU MUHSUSI NA WATUNZA KUMBUKUMBU KUSHIRIKI MKUTANO UTAKAOWAJENGEA UWEZO KIUTENDAJI KUTIMIZA DHAMIRA YA MHE. RAIS YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 16 Mei, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka waajiri katika Taasisi za Umma na Sekta Binafsi kuwaruhusu na kuwawezesha Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano wa kitaaluma Zanzibar uliolenga kuwajengea uwezo kiutendaji ili waweze kutimiza dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa watanzania pamoja na kuleta maendeleo katika taifa.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo Jijini Dodoma, wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari wenye lengo la kuwahimiza waajiri nchini kuwaruhusu Makatibu Muhsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano wa kitaaluma ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza ufanyike Zanzibar.

Mhe. Simbachawene amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha utendaji kazi katika Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi unakuwa uliotukuka na wenye lengo la kuwahudumia wananchi, hivyo amewahimiza waajiri kuwaruhusu Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano huo wa kitaaluma ili wapate ujuzi na maarifa ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. 

“Mheshimiwa Rais kwa kutambua umuhimu wa kada hizi za Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu katika utendaji wa shughuli za Serikali na Sekta Binafsi, alielekeza ufanyike mkutano mkubwa wa kitaaluma Zanzibar ili wapate fursa ya kula kiapo cha uadilifu na kujadili namna ya kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Mhe. Simbachawene amewahimiza waajiri katika sekta ya umma kuhakikisha idadi kubwa ya Makatibu Mahususi na Watunza Kumbukumbu wanashiriki mkutano huo na kugharamiwa, ili ushiriki wao uwe na tija kiutendaji pindi watakaprejea katika maeneo yao ya kazi.

Mhe. Simbachawene amesema mkutano huo utafanyika katika Viwanja vya Mao Tse Tung Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kaulimbiu ya mkutano huo ni Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri Sehemu za Kazi ni Chachu ya Maendeleo Kitaaluma” ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Mhe. Simbachawene amesema kuwa, maandalizi ya mkutano huo kwa kiasi kikubwa yamekamilika kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na hivisasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakamilisha maandalizi ili washiriki wote wanaokadiriwa kuwa 8000 wawe na ukakika wa kupata huduma za malazi na usafiri pindi watakapokuwa wakishiriki mkutano huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika  tarehe 27/11/2022      Jijini Arusha, alielekeza ufanyike mkutano wa pamoja Zanzibar wa TAPSEA na TRAMPA  utakaowawezesha kubadilishana uzoefu kiutendaji na kuweka mikakati endelevu na madhubuti ya kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) na Watendaji wa ofisi yake jijini Dodoma kuhusu Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano wa kitaaluma Zanzibar.


Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano wa kitaaluma Zanzibar.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu kushiriki mkutano wa kitaaluma Zanzibar.



Tuesday, May 16, 2023

MHE. SIMBACHAWENE AMFARIJI WAZIRI MKUU MSTAAFU, MHE. JOHN MALECELA KUFUATIA KIFO CHA MTOTO WAKE, BW. WILLIAM MALECELA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Malecela, Mtaa wa Kilimani jijini Dodoma kufuatia kifo cha mtoto wa Mhe. Malecela, Bw. William Malecelea kilichotokea tarehe 14 Mei, 2013. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mwenye suti ya kijivu) akiwa kwenye msiba wa mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Malecela. Kushoto kwake ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai. Wengine ni viongozi wa ofisi yake pamoja na waombolezaji.  



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mwenye suti ya kijivu) akimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Malecela (Wa kwanza kulia) alipoenda kumfariji nyumbani kwake Kilimani jijini Dodoma kufuatia kifo cha mtoto wake, Bw. William Malecela. Katikati ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.