Friday, January 29, 2016

Katibu Mkuu-Utumishi atembela Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA)

Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro, wa pili kulia, akijiandaa kushiriki kikao kwa njia ya video na wajumbe kutoka Chuo cha Utumishi Kenya. Kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa TaGLA Bw. Charles Senkondo. 
Mkutano kwa njia ya video ukiendelea kati ya Katibu Mkuu Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro na washiriki kutoka Chuo cha Utumishi Kenya (katika video).

Sehemu ya Maafisa Rasilimaliwatu wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi -Bw. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani)

Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (kulia) akiangalia moja ya chumba cha mafunzo

Monday, January 25, 2016

Serikali yafungua rasmi mafunzo ya ukusanyaji Taarifa za Tathmini ya Kazi

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kufungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akifungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

Timu ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi baada ya kufungua mafunzo kwa timu hiyo kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. Waliokaa kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

Thursday, January 21, 2016

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZUNGUMZA NA MINIBUZZ TV KUHUSIANA NA MASUALA YA KIUTUMISHI

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kulia) akisikiliza swali la Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano kuhusiana na masuala ya kiutumishi yaliyofanyika ofisini kwake 

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake 

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake 

Thursday, January 14, 2016

TAARIFA YA MSIBA


MHE. KAIRUKI ATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alipoitembelea taasisi hiyo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Taasisi ya Uongozi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wednesday, January 13, 2016

Waziri Kairuki azungumza na viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb)akizungumza na Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-Utumishi pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi katika kikao kazi kati yake na viongozi hao. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb)akizungumza na Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-Utumishi pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi katika kikao kazi kati yake na viongozi hao.

Mhe. Kairuki atembelea Mfuko wa Rais wa Kujitegemea

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) (kushoto)  akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haighat Kitala (kulia) alipotembelea ofisi hiyo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb)(kulia)  akizungumza na vyombo vya habari alipotembelea Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) . 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF)  alipotembelea ofisi hiyo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) akipokea Nyaraka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haighat Kitala (kulia) alipotembelea ofisi za Mfuko huo. 

Tuesday, January 5, 2016

Mhe. Kairuki aitembelea Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisalimiana na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo.   

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Salome S.Kaganda (kushoto) alipotembelea ofisi hiyo

MHE. KAIRUKI AKUTANA WATUMISHI WA OFISI YAKE,AMKARIBISHA KATIBU MKUU MTEULE

Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi hao.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. HAB Mkwizu akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Tixon Nzunda akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Mhe. Waziri na watumishi wa ofisi hiyo

 Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda.

Katibu Mkuu mteule Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro (kushoto) akipokea Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) kutoka kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu (kulia). Anayeshuhudia ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Tixon Nzunda.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi akila kiapo cha utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt.Laurian Ndumbaro akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Monday, January 4, 2016

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA YA KIKAZI TAKUKURU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisalimiana na watumishi wa TAKUKURU alipotembelea ofisi hiyo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa TAKUKURU (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hiyo.

Mtumishi wa TAKUKURU akiuliza swali kwa Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati Waziri alipokuwa akizungumza na watumishi wa TAKUKURU. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akipokea Nyaraka kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola alipotembelea ofisi za TAKUKURU.