Monday, July 18, 2016

MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA WABUNIFU NA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Pwani ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na watumishi wa Mkoa wa Pwani (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. 

Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. 

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Bw. Yusuph Kipengele akiwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bwana Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Pwani.


Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bi. Christina Hape akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Pwani. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP. Ibrahim Mahumi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bwana Issa Ng’imba.


Friday, July 15, 2016

MHE. KAIRUKI AKUTANA NA WATUMISHI MKOA WA MOROGORO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiongea na Viongozi wa mkoa wa Morogoro (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na viongozi hao kilichofanyika tarehe 15/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kabla ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 15/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akifuatilia taarifa ya mkoa wa Morogoro ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 15/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru.

Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kilichofanyika tarehe 15/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro

Waziri waNchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. AngellahKairuki (Mb) amewataka Watendaji wa Taasisi za Serikali kusimamia suala zima la watumishi na wadau kupata mrejesho wa barua wanazozituma kwenye taasisi zao.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo leo wakati wa kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mhe. Kairuki amesema kumekuwa na malalamiko mengi sana ya watumishi na wadau kutopata mrejesho wa barua wanazozituma kwenye taasisi za Serikali na hata wakijibiwa sio kwa wakati.

“Tunataka barua zijibiwe mara tu mzipatapo, hata kukiri kupokea pia ni mrejesho hivyo ni vema tukajibu barua na kwa wakati”Mhe. Kairuki alisisitiza.

Aidha, Mhe. Kairuki amewaagiza Watendaji hao kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye masija la za ofisi zao ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Amesema eneo la ofisi za Masijala limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kwa majalada kutoonekana na kusababisha watumishi na wadau kutopata mrejesho.
“Tutoe mwongozo kwa watumishi wa Masijala na tusiwaache bila kuwafuatilia kwani eneo hili limekuwa likilalamikiwa sana. Ikiwezekana tufanye kaguzi za kushtukiza ili kuleta ufanisi katika kazi” Mhe. Kairuki aliongeza.

Ameongeza kuwa ufuatiliaji pia ufanyike kwa kila Ofisa ambaye anakaa na jalada kwa muda mrefu bila kutoa mrejesho.

Mhe. Kairuki amekutana na watumishi wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa ziara alizozipanga kuzitekeleza mikoani kwal engo la kusikiliza kero za watumishi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuangalia ni namna gani ya kuweza kuboresha utendaji kazi Serikalini.

Thursday, July 14, 2016

UTUMISHI YATOA UFAFANUZI KUHUSU MASUALA MBALIMBALI YA KIUTUMISHI KATIKA KIPINDI CHA MORNING TRUMPET KINACHORUSHWA NA AZAM TV

Mtangazaji wa Kipindi cha “Morning Trumpet” kinachorushwa na AZAM TV,  Bw. Faraja Sendegeya (kushoto)  akifanya mahojiano na Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bw. Mathias Kabunduguru – Mkurugenzi wa Undelezaji Sera (katikati) na Bw. Nyakimura Muhoji - Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma.  Kipindi hicho kililenga kutoa elimu kwa umma juu ya masuala mbalimbali ya kiutumishi na kilirushwa mapema leo.

Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Kipindi cha “Morning Trumpet “ kinachorushwa na AZAM TV. Katikati ni Mkurugenzi wa Undelezaji Sera wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathias Kabunduguru na kushoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Faraja Sendegeya. 

Mkurugenzi wa Undelezaji Sera wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathias Kabunduguru akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Kipindi cha “Morning Trumpet “kinachorushwa na AZAM TV.  Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kushoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Faraja Sendegeya.

Tuesday, July 12, 2016

Waziri wa Utumishi wa Zanzibar Mhe.Haroun Suleiman amtembelea Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Kairuki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipomtembelea ofisini kwake. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman (kulia) akisisitiza jambo, wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ofisini kwake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipomtembelea ofisini kwake.

MATUKIO: ZIARA YA MHE. KAIRUKI MKOANI TANGA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifuatilia taarifa ya mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi, Utawala Na Rasilimaliwatu, Bwana Bernard Marcelline wakati wa kikao kazi na Viongozi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela na kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Injinia Zena Said.
Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bwana Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.


Monday, July 11, 2016

Mhe. Kairuki ataka Watumishi kushirikishwa katika Nyaraka mbalimbali zinazotolewa na SerikaliWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Injinia Zena Said wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na watumishi wa mkoa wa Tanga (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akisikiliza maoni ya watumishi wa mkoa wa Tanga (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela na Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Injinia Zena Said.

Ofisa Mwendeshaji kutoka GEPF mkoani Tanga, Bwana, Erick Haule akitoa maoni wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, Bwana John Mahali, akitoa maoni wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb), amewataka Watendaji wa Taasisi za Serikali kuwashirikisha watumishi katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Waziri Kairuki aliyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa mkoa wa Tanga katika kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mhe. Kairuki amesema ni vema watumishi wakashirikishwa katika nyaraka hizo muhimu ili waweze kujua nini kinaendelea katika Serikali yao wakiwa kama watumishi wa umma.
“Nyaraka hizi zimetengenezwa kwa ajili yao hivyo kukaa kimya bila kuwashirikisha si sawa kwani nao wanapaswa kujua ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” Mhe. Kairuki aliongeza.
Amesema kumekuwa na mabadiliko mengi katika miundo lakini watumishi hawafahamu kwasababu hawashirikishwi.
Aidha, Mhe. Kairuki amewataka Watendaji hao kutenga muda angalau mara moja kwa mwezi ili kusikiliza malalamiko na kero za watumishi.
“Watumishi wengi wamekuwa wakinyanyasika sana lakini wanashindwa pa kusemea hivyo ni vema tukatenga muda wa kusikiliza wanakumbwa na changamoto zipi,” aliongeza.
Ameongeza kuwa kusikiliza kero za watumishi mara kwa mara kutasaidia kupunguza malalamiko mengi na watumishi kufanya kazi kwa bidii hivyo kuongeza pato la taifa.

Ziara ya Mhe. Kairuki mkoani Tanga, ni mwendelezo wa utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi katika mikoa mbalimbali nchini kusikiliza kero na malalamiko ili kuweza kuyafanyia kazi. Kabla ya kukutana na watumishi wa Mkoa wa Tanga, Mhe, Kairuki ameshakutana na watumishi wa mikoa ya Singida, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara.

Tuesday, July 5, 2016

SERIKALI YAFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwatangaza Makatibu Tawala wa Wilaya wateule katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais - Utumishi. kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro. 

Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipokuwa akiwatangaza  Makatibu Tawala wa Wilaya wateule katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais - Utumishi 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais - Utumishi 

Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipokuwa akiwatangaza  Makatibu Tawala wa Wilaya wateule katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais - Utumishi