Wednesday, June 28, 2023

SIKUKUU NJEMA YA EID-AL-ADHA

 


SIKUKUU NJEMA YA EID-EL-ADHA

 


SIKUKUU NJEMA YA EID-AL-ADHA

 


SIKUKUU NJEMA YA EID-AL-ADHA

 


WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Sehemu ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watendaji hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Aliyesimama) akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Meza kuu katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Katikati) na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia) wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa maua ya ukaribisho wakati alipowasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea maua ya ukaribisho mara baada ya kuwasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya  watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya  watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Dodoma.


Naibu Katibu, Idara ya Ajira, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Lucas Mrumapili akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti hiyo ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na watumishi hao kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


















Friday, June 23, 2023

WAZIRI MHE. SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUZINGATIA MIKATABA YA HUDUMA KWA MTEJA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA

 Na. Lusungu Helela-Dodoma

Tarehe 23 Juni, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wananchi huku akizitaka Taasisi zote za Umma kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Mteja kwani ni nyenzo na kiungo muhimu katika kuboresha utendaji kazi kati ya Serikali na Wananchi inaowahudumia.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 23, 2023 wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki  kwenye Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Mhe. Simbachawene amewataka Watumishi hao kutambua kuwa wanapotoa huduma bora kwa wananchi wanamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza suala hilo mara kwa mara.

Kufuatia hatua hiyo, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia Mikataba ya Huduma kwa Mteja katika utoaji wa huduma kwa wananchi ili haki na wajibu wa pande zote mbili utendeke kwa watoa huduma na wapokea huduma ambao ndio wateja.

Ameongeza kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kusimamia mifumo na viwango vya utendaji kazi Serikalini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na moja ya mifumo na viwango  vya Utendaji Kazi huo ni Mkataba wa Huduma kwa Mteja.

Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ni moja ya hatua muhimu ya kuboresha huduma bora kwa wananchi ambapo amesema jumla ya Mikataba ya Huduma kwa Mteja 34 ya Taasisi za Umma imeweza kuzinduliwa.

"Uzinduzi wa mikataba hii ya Huduma kwa mteja inakwenda kuwezesha watumishi wa umma kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati" amesema Mkomi

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ametumia fursa hiyo kuzipongeza Taasisi za Umma ambazo zimeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye maeneo yao kama ilivyoelekezwa na Ofisi yake.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daudi Kandoro akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mikataba hiyo  kwa niaba ya Wakuu wa Taasisi, amesema  watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa huku akiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilichoandikwa katika mikataba hiyo ili wananchi waweze kujua wajibu na haki zao.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki  kwenye Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Juma Mkomi akizungumza wakati wa Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Xavier Daudi  akizungumza wakati wa Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akimkabidhi  Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi  cheti cha  kuwa Mkataba wa Huduma  kwa Mteja uliokidhi viwango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakati wa Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine  akiiaga kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

 


 


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika  Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akifurahia jambo na Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Juma Mkomi wakati wa Uzinduzi  wa Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa na baadhi ya Watumishi wakifurahi mara baada ya kuzindua Mikataba ya Huduma  kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho Wiki ya  Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akizungumza wakati wa utoaji vyeti na Tuzo mbalimbali kwa Taasisi za Umma wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo Kitaifa yamnefanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.






Saturday, June 17, 2023

SERIKALI YATOA RAI KWA WATUMISHI WA UMMA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Na. Lusungu Helela-Dodoma

Tarehe 17 Juni, 2023 

Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa rai kwa Taasisi Simamizi na Vyama vya Kitaaluma kuhimiza na kuwasimamia watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.                     

Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Watalaamu Waandamizi wa Taasisi Simamizi na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi. 

Bi. Shuli amesema kumekuwa na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi katika sekta ya afya, manunuzi, ujenzi pamoja na elimu ambayo yanahusu uvunjifu wa maadili, hivyo anaamini mafunzo hayo waliyoyapata kwa muda wa siku mbili yatasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

Kufuatia hatua hiyo, Bi. Shuli amezitaka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kujenga imani kwa wananchi na kuonesha thamani ya fedha zinazowekezwa na serikali katika miradi mbalimbali kwa kuwasimamia ipasavyo wataalamu wao katika utendaji kazi wao wa kila siku

‘’Ni matarajio yetu kupitia mafunzo haya tutakuwa na utumishi uliotukuka kwa kuwa na Watumishi wa Umma wenye kuzingatia weledi na wachapa kazi ili kuendelea kulinda taswira nzuri ya serikali ’’ amesema Mwakilishi wa Katibu Mkuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika amesema kikao kazi hicho kimewapa fursa ya kubadilishana uzoefu katika nyanja ya usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma pamoja na kujadili mikakati mbalimbali itakayowasaidia kusimamia suala la maadili kwa watumishi wa umma.

"Katika kuhakikisha suala hili linakuwa endelevu tumeweka mikakati ya pamoja kwa lengo la kuhakikisha suala la maadili katika utumishi wa umma linasimamiwa ipasavyo" amesisitiza Bi. Mavika.  

Naye Afisa Muuguzi kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Rehema Msanjila amesema mafunzo aliyoyapata yataenda kuleta mapinduzi makubwa katika eneo analolifanyika kazi ikizingatiwa sekta ya afya imekuwa ikilalamikiwa sana katika uvunjifu wa maadili.

“Nina imani kubwa kutokana na mikakati mikubwa tuliyojiwekea katika kikao hiki, tunakwenda kuwa na wauguzi na madaktari wenye kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi katika hospitali zetu hapa nchini’ amesema Bi. Msanjila.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli akizungumza Jijini Dodoma na Maafisa Waandamizi wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.


Mkurugenzi  wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.

Sehemu ya Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika kwa muda wa siku mbili jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.

Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni kutoka Baraza la Ukunga na Maadili Tanzania, Bi. Jane Mazigo akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli baada ya kufunga kikao kazi cha Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.


Afisa Muuguzi kutoka Baraza la Ukunga na Maadili Tanzania, Bi. Rehema Msanjila akielezea faida walizozipata katika kikao kazi cha kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi na jinsi kitakavyoenda kuleta mapinduzi ya kimkakati.

 


 

WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA

 


Friday, June 16, 2023

SERIKALI YAZIDI KUWEKA MIKAKATI KATIKA KUIMARISHA MAADILI KWA WATUMISHI WA UMMA

 Na. Lusungu Helela-DODOMA

Tarehe 16 Juni, 2023

Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema itaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha uadilifu, uwajibikaji na utawala bora katika Utumishi wa Umma ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa maendeleo ya taifa.                 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama hivyo  vya Kitaaluma vina jukumu kubwa la kusimamia dhana ya utawala bora nchini  ili kuongeza uwazi na uwajibikaji zaidi katika Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.

"Utawala bora, ni ile dhana inayozingatia maslahi mapana ya taifa, hivyo ninyi Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma muhakikishe huduma mnazozitoa zinazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji, haki sawa, demokrasia na kuwasikiliza watu wengi na wachache" amesisitiza Bw. Ngangaji.

Amefafanua kuwa, utaratibu wa kuwakutanisha Wataalamu hao  kutasaidia kutoa mapendekezo ya namna ya kubadilisha na kuboresha Miongozo ya Usimamizi wa Maadili kwenye Taasisi hizo katika kusimamia dhana ya utawala bora nchini.

Katika hatua nyingine Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewataka wasimamizi hao wa maadili kuhakikisha wanawachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao wanakiuka maadili huku akisisitiza kuwapongeza na kuwatia moyo watumishi ambao wanafanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi  wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika amesema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kubaini changamoto za usimamizi wa maadili ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kusimamia maadili kutokana na uzoefu wanaokutana nao.

"Sisi tunaangalia maadili katika masuala ya Utumishi wa Umma lakini kwa wenzetu waliopo kwenye Vyama vya Kitaaluma wanaangalia madili ya kitaaluma kwani wapo Watumishi wa Umma ambao ni wanachama wa vyama hivyo" amesisitiza Bi. Mavika 

Akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji, Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Baraza la Uuguzi na Ukunga, Bi. Jane Mazigo amesema kikao hicho ni muhimu kwao kama wadau muhimu wa usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Utumishi wa Umma katika Vyama vya Kitaaluma hivyo, anaamini kitatoa mwelekeo mpya katika kuhakikisha wanabadilishana uzoefu  kutokana na changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji akizungumza Jijini Dodoma  na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika na upande wa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo.

Mkurugenzi  wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji kuzungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.


Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi .


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa waandamizi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.


Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kuzungumza nao kwenye kikao kazi na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.    


Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.