Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 15 Juni, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka ofisini na kwenda sehemu ambako huduma za kijamii zinatolewa kwa kuwa huko kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu kutondewa haki katika kupata huduma.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Watumishi wa Taasisi hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.
Amesema ni wakati sasa wa TAKUKURU kwenda kupambana na rushwa katika maeneo hayo badala ya kukaa ofisini huku wakisubiri kupewa taarifa za rushwa na watu wengine.
"Naitaka TAKUKURU ya sasa iende huko kwa wananchi wasio na sauti wanakopatiwa huduma za kijamii zikiwemo ardhi, elimu, afya na nyinginezo lakini kuna kero kubwa ya rushwa," Mhe.Simbachawene amesisitiza.
Ameongeza kuwa chombo hiki cha TUKUKURU kinatakiwa kiende sehemu zinakotolewa huduma za kijamii na kionekane kinafanya kazi ya kusikiliza, kunusa, kutazama, kugusa na kuwabaini wale wote wanaojenga mazingira ya rushwa kwa wananchi ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Yapo maeneo mengi ambayo tumeyaona ni ya kawaida lakini yanasababisha watoa huduma wetu kuingia katika rushwa, mangúniko ni mengi juu ya rushwa, hivyo ni lazima hatua zichukulie kudhibiti hili kwa maendeleo ya taifa,” Mhe Simbachawene amesema.
Aidha, Mhe. Simbachawene amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kikamilifu, hivyo ni wakati sasa wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais kwa kufanya kazi kikamilifu katika kupamba na rushwa na kuitokomeza.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, CP Salum Hamduni
amesema TAKUKURU imeanza kufanya kazi zake kimkakati kutoka kufanya kazi
kimazoea hadi kwenye kuhakikisha wananchi wanapewa huduma za kijamii pasipo
kutengenezewa mazingira ya rushwa.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza
na Maafisa wa TAKUKURU wakati alipowatembelea katika ofisi zao zilizopo jijini
Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya Maafisa wa TAKUKURU wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati alipowatembea katika ofisi zao zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la
kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
kuzungumza na Maafisa wa TAKUKURU Katika ofisi zao zilizopo jijini Dodoma kwa
lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakati alipowatembelea katika ofisi za TAKUKURU zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema
Mwakalyelye akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wake Mhe.
Ridhiwani Kikwete kwa kufanya kikao kazi na Maafisa wa TAKUKURU kwa lengo la
kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya
pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa wa TAKUKURU alipowatembelea katika ofisi za Dodoma kwa lengo la kuhimiza
uwajibikaji.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipokea nakala ya Mwongozo wa
TAKUKURU Rafiki kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni wakati
wa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete moja ya vitendea kazi vya TAKUKURU kutoka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
CP. Salum Hamduni wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete wakiwa wamekabidiwa maua
ikiwa ni ishara ya ukaribisho wao katika ofisi za Dodoma za TAKUKURU.
No comments:
Post a Comment