Tarehe 03 Juni, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
amewataka wahitimu wa kozi
mbalimbali katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)
kufahamu kuwa utumishi wa umma ni ibada, hivyo watakapopata fursa ya kuajiriwa
katika taasisi za umma itawapasa kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu na
kujitoa katika kuwahudumia wananchi ili kutimiza ibada hiyo kwa maendeleo ya
taifa.
Mhe. Simbachawene ametoa nasaha hizo kabla ya
kuwatunuku wahitimu wa kozi
mbalimbali katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika Mkoani Tanga.
Mhe.
Simbachawene amesema, utumishi wa umma umelenga katika kuwahudumia wananchi na
sio sehemu ya kutengeneza faida, hivyo wahitimu hao watakapopata fursa ya
kuajiriwa serikalini ni lazima wazingatie hilo.
“Kuna
tofauti sana kati ya mtumishi anayeajiriwa katika utumishi wa umma na mtumishi
anayetumikia sekta binafsi, utumishi wa umma ni ibada na kujitoa, kwenye
utumishi wa umma tunahudumia wananchi lakini kwenye sekta binafsi wao
wanatengeneza faida, utumishi wa umma unahitaji unyenyekevu katika kuwahudumia
wananchi na sio sehemu ya kujitafutia masilahi binafsi,” Mhe. Simbachawene
amesisitiza.
Ili kuwa na watumishi walio na maadili, Mhe. Simbachawene ameusisitiza uongozi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kutilia mkazo katika kusimamia na kufundisha maadili jambo ambalo litasaidia pia kuwatengeneza watumishi wenye uvumilivu watakaoweza kufanya kazi na kuwahudumia wananchi sehemu yoyote watakayopangiwa bila kuwa na manungĂșniko.
Kutokana na changamoto nyingi za kiutumishi zilizopo, Mhe. Simbachawene ameulekeza uongozi huo wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, kufanya tafiti za masuala mbalimbali ya kiutumishi ambazo zitawawezesha Viongozi wa Nchi kufanya maamuzi sahihi yanayohusiana na maendeleo ya utumishi wa umma.
Mhe. Simbachawene amesema Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, ndicho chenye jukumu la kufanya utafiti wa masuala mbalimbali ya kiutumishi, hivyo wanatakiwa kuwekeza kwenye kufanya utafiti na kuandika taarifa zitakazotumiwa na viongozi kufanya maamuzi ya kisera na kisheria ili kuboresha utumishi wa umma kwani huwezi kufanya maamuzi bila kufanya tafiti.
Katika kuhakikisha wanachuo wa Chuo cha Utumishi wa
Umma Tanzania, Kampasi ya Tanga, wanapata elimu katika mazingira mazuri kama
ilivyo katika Kampasi nyingine za chuo hicho, Mhe. Simbachawene amewaelekeza Watendaji wa Ofisi yake kwa
kushrikiana na Uongozi wa Mkoa wa Tanga kutafuta eneo zuri ambalo wanachuo
watapata nafasi ya kujifunzia tofauti na la sasa ambalo majengo yake
hayaridhishi.
Aidha,
Mhe. Simbachawene ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Tanga na wananchi wa mkoa huo
kwa kuona umuhimu wa elimu na kuamua kutoa eneo la Maweni ambalo Kampasi ya
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania itajengwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe. Hashim Mgandilwa ameipongeza Serikali kwa uamuzi
wake mzuri wa kuanzisha Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini
Tanga kwani itasaidia kuleta chachu kwa wazazi na familia ambazo zinaishi
ukanda wa Pwani kupata mwamko wa elimu.
Kwa
Upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejiementi ya Utumishi wa Umma, Bw.
Juma Mkomi amewasihi wahitimu kuzingatia uadilifu na utendaji mzuri
watakapopata fursa ya kuajiriwa katika utumishi wa umma na hata katika sekta
binafsi kwani uadilifu unahitajika katika maeneo yote kwa manufaa ya nchi.
Bw. Mkomi amesema yeye akiwa ndiye Mtendaji wa Ofisi ya Rais -UTUMISHI atazifanyia kazi changamoto zote za Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ikiwemo ya kukamilisha utaratibu wa upatikanaji wa hati eneo la Maweni lililotolewa na Mkoa wa Tanga na wananchi ili kuanza kwa ujenzi wa Kampasi ya Tanga na kutafuta eneo ambalo wanachuo watapata fursa ya kujisomea katika hali yenye ubora.
Akiwasilisha taarifa kuhusu mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Ernest Mabonesho amesema jumla ya wahitimu 1,803 kutoka katika kampasi zote sita za TPSC ambazo ni Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Tabora, Singida na Mbeya wametunukiwa vyeti katika ngazi ya shahada, stashahada na astashahada katika kozi mbalimbali.
Sehemu ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika
mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakiwa kwenye maandamano
wakati wa mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika
mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka na Watendaji wa Ofisi yake kabla ya kuanza kwa maandamano ya mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisindikiza maandamano ya wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika mkoani Tanga. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mhe Hashim Mgwandila akitoa salamu za Mkoa wa Tanga
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa mahafali ya 37 ya Chuo
cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika mkoani Tanga.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa maelezo mafupi kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wahitimu wa kozi
mbalimbali katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
yaliyofanyika mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka akitoa neno la utangulizi wakati
wa mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Tanga.
Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo
cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuhusu mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma
yaliyofanyika mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitunuku cheti kwa
mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao wakati wa mahafali ya 37
ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha
ya pamoja na mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, Bw. Daudi Kingazi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Kampasi ya Tanga mara baada ya kuhitimisha mahafali ya 37 ya
Chuo cha Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiimba kwaya na
wanakwaya wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Tanga wakati wa
mahafali ya 37 ya Chuo cha Utumishi wa Umma yaliyofanyika mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment