Na. Lusungu Helela-Dodoma
Tarehe 23 Juni, 2023
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wananchi
huku akizitaka Taasisi zote za Umma kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Mteja kwani
ni nyenzo na kiungo muhimu katika kuboresha utendaji kazi kati ya Serikali na
Wananchi inaowahudumia.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 23, 2023 wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mhe. Simbachawene amewataka Watumishi hao kutambua kuwa wanapotoa huduma bora kwa wananchi wanamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza suala hilo mara kwa mara.
Kufuatia
hatua hiyo, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia Mikataba ya Huduma kwa Mteja katika
utoaji wa huduma kwa wananchi ili haki na wajibu wa pande zote mbili utendeke kwa
watoa huduma na wapokea huduma ambao ndio wateja.
Ameongeza
kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kusimamia mifumo na viwango vya utendaji kazi
Serikalini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa
wananchi na moja ya mifumo na viwango
vya Utendaji Kazi huo ni Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Awali,
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema
uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ni moja ya hatua muhimu ya kuboresha
huduma bora kwa wananchi ambapo amesema jumla ya Mikataba ya Huduma kwa Mteja
34 ya Taasisi za Umma imeweza kuzinduliwa.
"Uzinduzi wa mikataba hii ya Huduma kwa mteja inakwenda kuwezesha watumishi wa umma kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati" amesema Mkomi
Aidha,
Katibu Mkuu Mkomi ametumia fursa hiyo kuzipongeza Taasisi za Umma ambazo
zimeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye maeneo yao kama ilivyoelekezwa na
Ofisi yake.
Naye,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daudi Kandoro akitoa
neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mikataba hiyo kwa niaba ya Wakuu wa Taasisi, amesema watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa huku
akiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilichoandikwa katika mikataba hiyo
ili wananchi waweze kujua wajibu na haki zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza na watumishi mbalimbali wa
Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Uzinduzi wa
Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha
Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika
Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw.Juma Mkomi akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya
Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho Wiki
ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere
Square Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Bw.Xavier Daudi akizungumza wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika
Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi cheti cha kuwa Mkataba wa Huduma
kwa Mteja uliokidhi viwango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za
Umma katika Kilele cha Maadhimisho wiki ya Utumishi wa Umma ambayo
kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi
wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma
katika Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo
kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Mhe.Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine akiiaga kwaya ya Chuo
cha Utumishi wa Umma mara baada ya Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma
kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho wiki ya
Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square
Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika
Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akifurahia jambo na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Juma Mkomi wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa na baadhi ya Watumishi wakifurahi
mara baada ya kuzindua Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele
cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika
katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji
wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akizungumza wakati wa utoaji vyeti na Tuzo
mbalimbali kwa Taasisi za Umma wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma ambayo Kitaifa yamnefanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment