Tuesday, February 23, 2016

UTUMISHI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MFUMO SHIRIKISHI WA TAARIFA ZA KIUTUMISHI NA MISHAHARA (HCMIS VERSION 9) KWA MAAFISA UTUMISHI WA WILAYA,MIKOA NA TAASISI ZA SERIKALIBaadhi ya Maafisa Utumishi kutoka Taasisi 16 za Serikali na Halmashauri za Wilaya 6 nchini wakifuatilia mafunzo ya Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS Version 9) yaliyofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) jijini Dar es Salaam.

Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Philemon Mbaga akitoa mafunzo kwa maafisa utumishi kutoka Taasisi 13 za Serikali na Halmashauri za Wilaya 6 nchini katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).

Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaendelea na Vikao kazi kwa Njia ya Video (Video Conference)

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (picha ndogo kulia) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video kilichohusisha Ofisi ya Rais-Utumishi,Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda, Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na ofisi za Sekretarieti za mikoa ya Iringa, Pwani, Mtwara, Dar es Salaam, Kagera,Kigoma.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Sakina Mwinyimkuu (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu Uimarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini kwenye kikao kazi kwa njia ya video kilichofanyika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).

Washiriki wa kikao kazi kwa njia ya video wakimsikiliza mtoa mada.

Monday, February 22, 2016

Waziri Kairuki amsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hatua ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) pamoja na  wakuu wa matawi ya chuo hicho ya Dar es salaam na Tabora.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake kuhusu hatua ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Said Nassoro. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bi. Suzan Mlawi, kulia ni Menejimenti ya TPSC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake kuhusu hatua ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Said Nasoro (wa pili kutoka kushoto mbele) pamoja na  wakuu wa matawi ya chuo hicho ya Dar es salaam na Tabora.

Wednesday, February 17, 2016

UTUMISHI YAPOKEA WATAALAM WATANO WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPAN

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) akizungumza na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliokuja kutoa huduma katika sekta ya viwanda,elimu na afya waliporipoti ofisi za Utumishi. 
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathias Kabunduguru (katikati mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliokuja kutoa huduma katika sekta ya viwanda,elimu na afya 

Thursday, February 11, 2016

Balozi wa Korea nchini akutana na Mhe. Kairuki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na ujumbe kutoka ubalozi wa Korea nchini ulipomtembelea ofisini kwake.

Wednesday, February 10, 2016

MHE. KAIRUKI ATEMBELEA MKURABITA

Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa MKURABITA wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea ofisi hiyo

Mratibu wa Mpango MKURABITA Bi. Seraphia R. Mgembe (kushoto) akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (katikati) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa MKURABITA alipoitembelea ofisi hiyo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwa katika kikao na watumishi wa MKURABITA alipoitembelea ofisi hiyo . Wengine ni waandishi wa habari walioudhuria katika tukio hilo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watumishi wa MKURABITA alipoitembelea ofisi hiyo 

Wednesday, February 3, 2016

Monday, February 1, 2016

DAWATI LA MSAADA (HELP DESK)


Katibu Mkuu-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro atembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakimsikiliza Katibu Mkuu-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ofisini hapo.
Katibu Mkuu-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao na Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakimsikiliza Katibu Mkuu-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ofisini hapo.