Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa kazini akipitia taarifa za Mtumishi wa Umma mkoani Kagera . (Picha ya Maktaba) |
Kuondoa Watumishi wasiostahili katika orodha ya malipo ya mshahara Serikalini ni kazi endelevu na inafanyika kwa kushirikiana na waajiri nchini. Katika makala hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) anaongea kuhusu hatua mbalimbali na kazi zilizofanywa na Ofisi yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alisema hayo hivi karibuni katika kipindi
cha mahojiano ya moja kwa moja katika Runinga ya Taifa (TBC) na kusisitiza
waajiri wanawajibu wa kuondoa mtumishi yeyote asiyestahili mara moja.
“
Tumefanya zoezi mahsusi kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi
wasiostahili. Watumishi wanaoondolewa ni
wale walioacha kazi, kufukuzwa kazi, kumalizika kwa muda wa ajira ya mkataba na
kugombea nafasi za kisiasa. Kuanzia tarehe 01 Machi, 2016 hadi tarehe 20
Agosti, 2016 jumla ya watumishi 16,127 wameondolewa na wasingeondolewa
kwa wakati wangeisababishia Serikali
hasara ya Shilingi 16,014,697,390 kwa mwezi mmoja” Mhe. Kairuki aliainisha.
Alisema
hatua zinachukuliwa kwa wote waliobainika kuhusika katika suala hilo ambapo hadi
tarehe 20 Agosti, 2016 jumla ya watumishi
839 walifikishwa Polisi na TAKUKURU ili kutoa maelezo; na uchunguzi unaendelea hatimaye hatua za kisheria
zichukuliwe kulingana wa ushahidi
utakaopatikana.
Waziri
Kairuki alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba fedha zote zilizolipwa
kwa watumishi wasiostahili zinarejeshwa Serikalini akibainisha kuwa toka mwezi
Machi, 2016 hadi mwezi Julai, 2016 jumla fedha zilizorejeshwa ni Shilingi
14,403,046,089.27 na zoezi ni endelevu.
Waziri
Kairuki alisema Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCIMS)
unaimarishwa kulingana na mahitaji na kutaja maeneo yaliyoimarishwa ikiwamo; Uwezo
wa kutambua na kuzuia kuajiriwa watu wenye majina yanayofanana; Kuongeza moduli
ambayo inamwezesha mwajiri kufanya uhakiki wa watumishi kwa kutumia taarifa
mbalimbali zikiwemo za Kitambulisho cha Taifa; Uwezo wa kuwaondoa kwenye orodha
ya malipo ya mishahara watumishi waliofikisha umri wa kustaafu na ambao hawana
mikataba; Kuongeza Moduli ya Utambuzi wa Kituo cha Kazi cha mtumishi (Service Delivery Point) na hilo limeanza
kwa Idara za Afya, Elimu, Kilimo na Mifugo; na Wigo wa matumizi ya mfumo
umepanuliwa ili kuwawezesha Wakuu wa Idara za Afya, Elimu (Sekondari/Msingi),
Kilimo na Mifugo kutumia na kuona taarifa za watumishi walio chini yao.
Akiongea kuhusu mkakati wa kuboresha Maadili katika Utumishi wa Umma
alisema
pamoja na mambo mengine Serikali
inasimamia kukuza uelewa wa Maadili kwa Watumishi wa Umma kupitia mafunzo
na kuendeleza ushiriki wa Asasi za Kiraia (AZAKI) katika kuhamasisha wananchi kuzingatia
maadili na kuacha kutoa vishawishi kwa watoa huduma. Pia, kuhakikisha kila
Taasisi ya Umma ina Mkataba wa Huduma kwa Mteja na dawati la kupokea, kushughulikia
malalamiko na kutoa mrejesho kwa wananchi.
Waziri
Kariuki aliongeza pamoja na ofisi yake kuhakikisha Watumishi wa Umma wanatoa Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu
na kusimamia viapo hivyo, pia inaandaa Mfumo wa Kielektroniki unaojulikana kama
“Watumishi Portal” ambao utakuwa na
moduli ya kupokea malalamiko, maoni na kero mbalimbali kutoka kwa Watumishi wa
Umma na kuhamasisha Taasisi za Umma kuwa na kituo mahususi cha utoaji huduma (One Stop Service Centre) ili kupunguza
kero kwa wananchi wanaofuata huduma.
Eneo la Uwajibikaje
hali ikoje?
Waziri Kariuki alisema Serikali imekuwa na
utaratibu wa kupima utendaji wa Mtumishi Mmoja mmoja kwa kutumia Mfumo wa Wazi
wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS).
Hata hivyo, alisema “Serikali inalenga kuimarisha
mfumo wa uwajibikaji katika ngazi ya Taasisi ili kuhakikisha Taasisi za Umma
zinatekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuanzisha Mfumo wa Mikataba ya Utendaji
Kazi katika Taasisi zote za Umma kuanzia mwaka wa fedha 2017/18”.
Alifafanua
kuwa Mkataba huo ni makubaliano ya kimaandishi kati ya Taasisi za Umma na
Serikali ambayo yatatekelezwa na Taasisi husika katika kipindi cha mwaka mmoja
na Mkataba utajikita katika kupanga na kupima
utendaji wa Taasisi
na utakuwa na malengo, shabaha, vigezo na viashiria vya utendaji ambavyo
vitatekelezwa na Taasisi katika mwaka
husika.
Waziri
Kairuki alianisha kuwa Mkataba huo utaainisha wajibu wa Serikali katika
kuwezesha Taasisi kufikia malengo na shabaha na utekelezaji wake utafanyiwa
tathmini kila mwisho wa mwaka na matokeo yake kutangazwa kwa umma.
Miongoni mwa faida za mfumo huo ni kuziwezesha Taasisi za
Umma kuimarisha uchaguzi wa vipaumbele katika ngazi ya Taasisi na upangaji
mipango ya utekelezaji kila mwaka; kuimarisha ufuatiliaji na upimaji utendaji
kazi; na kuimarisha uwajibikaji na uwazi.
Usimamizi wa Maadili kwa
viongozi wa Umma ukoje?
Itaendelea...
kama zoezi la kuondoa watumishi hewa ni endelevu mbona bado kuna zuio la watumishi kuhama vituo vya kazi?
ReplyDeletendugu zangu tunaomba msaada wenu mturuhusu kuhama
ReplyDelete