Wednesday, January 30, 2019

SERIKALI MTANDAO YARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI KWA WAKATI

Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akifungua rasmi kikao kazi cha Serikali Mtandao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Serikali Mtandao wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo. 
Mkurugenzi Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango akitoa neno la shukrani na kuahidi kutekeleza maelekezo ya mgeni rasmi baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.
Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua rasmi kikao kazi cha Serikali Mtandao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.
Mkurugenzi Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wakala ya Serikali Mtandao pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Serikali Mtandao mara baada ya kufungua rasmi kikao kazi cha Serikali Mtandao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Friday, January 25, 2019

IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA YATAKIWA KUFUATILIA UTUNZAJI WA NYARAKA KWENYE TAASISI ZA UMMA ILI KUONDOA TATIZO LA UVUJAJI WA SIRI ZA SERIKALI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za serikali ili kuondokana na tatizo la uvujaji wa siri za serikali alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipata maelezo kutoka kwa  Mtunza Kumbukumbu Msaidizi, Bi. Joyce Maro juu ya kumbukumbu zilizohifadhiwa katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa alipofanya ziara ya kikazi katika Idara hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipata ufafanuzi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi katika utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika idara hiyo jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki kutoa nakala ya nyaraka ili kuihifadhi katika mfumo wa TEHAMA alipofanya ziara ya kikazi katika Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. Anayemsaidia kutoa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa alipofanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika idara hiyo jijini Dodoma. 

Wednesday, January 23, 2019

UJUMBE KWA VIONGOZI WA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA


SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU VIONGOZI WANAOKIUKA KIAPO CHA MAADILI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili  Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa ajili ya kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Mhe. Harold Nsekela. 
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Mhe. Harold Nsekela (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu majukumu ya ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.


Sunday, January 20, 2019

SEKRETARIETI YA AJIRA YATAKIWA KUTENDA HAKI ILI KUIWEZESHA SERIKALI KUPATA WATUMISHI WENYE SIFA STAHIKINaibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi  akieleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha  Naibu Waziri huyo na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo  Magogoni  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Magogoni katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu namna mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu inavyofanya kazi wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji.