Sunday, January 6, 2019

VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA MHE. MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA NA KUKUMBUKA MCHANGO ALIOUTOA KATIKA UJENZI WA TAIFA








Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipewa pole ya kufiwa na mama mzazi na  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipoenda kumfariji nyumbani kwake katika kijiji cha Nambunga wilayani Newala.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akipewa pole ya kufiwa na mama mzazi na  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko alipoenda kumfariji nyumbani kwake katika kijiji cha Nambunga wilayani Newala.

Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almasi Askofu Mstaafu Dkt. Mwachiko Boma, Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya Newala na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Mhe. Mkuchika kabla ya kumpumzisha  mama Tecla B. Mkuchika katika nyumba yake ya milele kijiji cha Nambunga Wilayani Newala.

Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kushiriki ibada ya mazishi ya Bibi Tecla B. Mkuchika ambaye ni mama mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na ndugu zake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiweka shada la maua  kwenye kaburi la  mama mzazi wa Mhe. Mkuchika, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwaongoza wanafamilia kuwasha mishumaa juu ya kaburi la Bibi Tecla B. Mkuchika, aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment