Sunday, January 13, 2019

TPSC YATAKIWA KUTOA MAFUNZO YATAKAYOWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA KUBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI

Add caption


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea  ofisini kwao makao makuu ya TPSC jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo, akieleza  majukumu ya TPSC kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TPSC cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua daftari la mmoja wa wanachuo wa Chuo cha Utumishi  alipowatembelea  wanafunzi  hao  katika moja ya madarasa  ya Kampasi ya Dar es Salaam. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwaasa wanachuo hao kusoma kwa bidii ili wawe watumishi wa umma bora hapo baadae.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akijaribu kutumia mashine ya kupiga chapa (typewriter) inayotumiwa kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa TPSC alipotembelea moja ya darasa katika Kampasi ya Dar es Salaam ya  Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania  jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwahimiza  wanachuo wa TPSC waliopo maktaba kutumia vema maktaba hiyo ya chuo kujisomea ili kuongeza  uelewa wa masomo wanayosoma,  alipoitembelea maktaba hiyo  iliyopo  Chuo cha Utumishi Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment