Tuesday, January 8, 2019

PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUWAPATIA MIKOPO KUNDI MAALUMU LA WALEMAVU, AKINA MAMA WAJASIRIAMALI NA VIJANA



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji  wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na  kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana  wakati wa ziara yake ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa  na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM  wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwasisitiza watumishi wa PTF kutoa huduma nzuri  kwa walengwa wa mikopo inayotolewa  na PTF wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

No comments:

Post a Comment