Sunday, January 20, 2019

SEKRETARIETI YA AJIRA YATAKIWA KUTENDA HAKI ILI KUIWEZESHA SERIKALI KUPATA WATUMISHI WENYE SIFA STAHIKI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi  akieleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha  Naibu Waziri huyo na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo  Magogoni  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Magogoni katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu namna mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu inavyofanya kazi wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji.

No comments:

Post a Comment