Saturday, March 30, 2024

HERI YA SIKUKUU YA PASAKA


 

WAZIRI SIMBACHAWENE AWASISITIZA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUTOA HUDUMA ZENYE VIWANGO KWA WANANCHI

 




Na Lusungu Helela-Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Ofisi yake kutoa huduma bora kwa wananchi kwa haraka na ufanisi, huku akisisitiza ubora wa huduma hizo uendane na uzuri wa jengo jipya ambalo Ofisi hiyo imehamia hivi karibuni.

 

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jana jioni mara baada ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo na kuwakutanisha Watumishi wote wa Ofisi hiyo wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

 

Amesema anatamani kuona wananchi na watumishi wanaohudumiwa katika jengo hilo jipya wanafurahia huduma wanazozipata kwani kitendo cha Watumishi kuhamia katika jengo hilo jipya kwa sasa kuna utulivu wa akili.

 

“Sasa watumishi wote tupo katika jengo moja, sitegemei kusikia visingizio vya hapa na pale kuwa jalada fulani halipo Mtumba bali liko Ofisi za UDOM kule ambako baadhi ya watumishi walikuwa wakifanya kazi, tufanye kazi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

 

Amesema kitendo cha Watumishi kuhamia katika jengo moja tofauti na ilivyokuwa mwanzo ni muhimu sasa kwa Watumishi wa Ofisi yake kushirikiana katika kufanya kazi ili kuhakikisha wateja wanaridhika na huduma wanazozipata.

 

"Serikali imejenga jengo zuri mno, hii kwenu ni motisha kubwa, hivyo hakikisheni huduma mnazozitoa ziwe za viwango vya hali ya juu ili kuendana na thamani ya jengo" amesema Mhe. Simbachawene.

 

Aidha, Mhe. Simbachawene ameiagiza Ofisi hiyo kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi kwa pamoja lengo likiwa ni kulinda afya pamoja na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

 

"Kwa sasa tupo jengo moja, naagiza utaratibu uandaliwe wa kufanya mazoezi kwa pamoja ili kulinda afya zetu na kuwahudumia wananchi ipasavyo" amesema Mhe.Simbachawene

 

Awali, Katibu Mkuu UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi alimshukuru Waziri Simbachawene kwa wazo la kuandaa Iftar hiyo huku akiwataka Watumishi wa Ofisi yake kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.

 

"Mtaungana nami, leo ni siku muhimu sana ambapo Waislamu mpo katika mfungo wa Ramadhani huku Wakristo mkiwa katika mfungo wa Kwaresma, tumekutana hapa ili kufuturu pamoja kuonyesha ishara ya upendo na ushirikiano," Bw. Mkomi amesisitiza.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la shukrani kwa Waziri Simbachawene amemuahidi kuwa maagizo yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu ikiwemo utamaduni wa namna hiyo wa kukutana kwa pamoja.



Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa  Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa katika mstari wakichukua futari jana jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akizungumza jana jioni na Watumishi wa Ofisi yake kabla  ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

 


Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi  akitoa neneo la shukrani kwa  jana jioni kwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mbele ya Watumishi wa Ofisi hiyo baada ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma


Sehemu ya Watumishi wakimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene  wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

 

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati)  akiwa na  Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kulia)  pamoja  na Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi ( kushoto) wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma  

Baadhi ya Maafisa wa  Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa katika mstari wakichukua futari jana jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma

 

Sehemu ya Watumishi wakiwa katika   Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

 

Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa  Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa na nyuso za furaha  jana jioni mara baada ya  Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo  ambapo Watumishi wote walikutanishwa  wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya  kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa  Serikali Mtumba Jijini Dodoma.


Tuesday, March 26, 2024

MARUFUKU HUJUMA BAINA YA WATUMISHI MAHALI PA KAZI

 Na.Lusungu Helela- Dodoma

Tarehe 26 Machi, 2024

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Juma Mkomi amewataka Watumishi katika ofisi yake kupendana na kuthaminiana mahali pa kazi huku akiwasihi kuacha tabia ya kuhujumiana.

Ametoa kauli hiyo leo Machi 26, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala  Bora kilichowakutanisha Watumishi hao pamoja na baadhi ya Wajumbe wa TUGHE Taifa. 

"Sisi ni jicho katika Utumishi wa Umma tujitahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana ili kutimiza malengo tuliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa watumishi na wananchi kwa jumla kwa haraka na kwa ufanisi " amesisitiza Mkomi.

Bw. Mkomi amewataka watumishi hao kupendana kwa kuwa sehemu kubwa ya muda wao unatumika kazini. Hivyo, mazingira ya kazi yanatakiwa kuwa na amani na utulivu ili ufanisi uongezeke na mwananchi aweze kupata huduma bora.

Vilevile, ametoa wito kwa Wakurugenzi wote kuwaandaa watumishi walio chini yao kwa ajili ya kurithishana madaraka na kuwapa majukumu watumishi hao ili kuwajengea uwezo kiutendaji na kuwafanya waoneshe uwezo wao kazini.

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi amewanyooshea vidole baadhi ya watumishi wenye tabia ya kuvujisha siri ambapo amewatahadharisha kuwa yeyote atakayebainika hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende ametumia fursa ya mkutano huo kuwaomba Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kuwasikiliza watumishi walio chini yao kwa kuwa wanaweza kuwa na mawazo mazuri yenye kujenga taasisi na Serikali kwa jumla.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi yake uliolenga kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma. 

Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Juma Mkomi (aliyekaa meza kuu) wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo uliolenga kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Julieth Magambo akiwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute.


Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Bw. Cosmas Ngangaji akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bw. Mussa Magufuli.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. 


Mwakilishi wa Katibu Mkuu-TUGHE, Bw. Nsubisi Mwasandende akiwasilisha hoja kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. 


Mjumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Shaha Nampeha akichangia moja ya hoja wakati wa mkutano huo uliolenga kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma


Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi yake mara baada ya kufungua mkutano huo uliolenga kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.

 





KUHAMA KWA OFISI


 

Sunday, March 24, 2024

KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25 YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

 


KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25 YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Na Lusungu Helela-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. 

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Machi 23, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati hiyo na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.  

Amesema baada ya majadiliano mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na bajeti iliyotengwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia. 

“Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” amebainisha Mhe. Kyombo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati hiyo kwa ushauri na kupitia bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ya kuboresha kabla ya kuiwasilisha kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.

“Mimi pamoja na timu yangu, tunatoa shukrani za dhati kwa jinsi mnavyotoa michango yenu yenye muelekeo wa kuboresha Utumishi wa Umma nchini ili kukidhi matakwa  na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Simbachawene.

 

 


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25. 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao  cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kilicholenga kuwasilisha tarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini  ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25 

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Juma Mkomi  akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao  cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zilizo zote  chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka, Bw. Firmin Msiangi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha  2024/25

 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akitoa ufafanuzi wa  hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha Kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  ya kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote  zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25

 

Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao  cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Watendaji wa ofisi hiyo wakati wa  uwasilishaji wa tarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zilizo zote  chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha  2024/25

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Mashimba Ndaki  akichangia hoja kuhusu masuala ya utumishi  wakati wa kikao  cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote  zilizo chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25

 


Tuesday, March 19, 2024

MAAFISA MASUULI WATAKIWA KUZINGATIA USHAURI WA WATAALAMU KATIKA TAASISI ZAO

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 19 Machi, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria kutoka katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kutoa ushauri mahususi kwa Maafisa Masuuli wao ili kuepuka kuipa hasara Serikali.

“Ninajua kusimamia rasilimaliwatu sio jambo jepesi kwani linahitaji hekima na busara. Wapo baadhi ya Maafisa Masuuli ambao hawasikilizi na hawapendi kupokea ushauri wa kitaalamu  kutoka kwa maofisa wao na hivyo kutoa uamuzi kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo kuipa hasara Serikali” amesema Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, iwapo sheria na kanuni za usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma hautazingatiwa, utaondoa adhima ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na utumishi wa umma unaotenda haki na wenye kuwajibika kwa umma.

Aidha, amebainisha kuwa, taasisi za umma zinapokuwa na malalamiko mengi ya watumishi ni ishara kuwa watendaji wa ofisi hizo hawafanyi kazi ipasavyo hata kama lalamiko liko ndani ya uwezo wao. Hivyo, kitendo cha kupeleka malalamiko hayo katika ngazi za juu kwa utatuzi ni dhihaka kwa utawala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi amesema Maofisa hao ni washauri wakuu wa Maafisa Masuuli katika taasisi zao, hivyo wanatakiwa kutoa ushauri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili kuepuka kuumiza watumishi.

Bw. Mkomi amewasihi maofisa hao kuhakikisha wanatatua matatizo ya watumishi wa umma kwa kuwasikiliza na wakati mwingine kuwaonya kwanza kuliko kuwafukuza katika utumishi wa umma jambo.

Awali, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Hilda Kabissa amesema kikao kazi hiki kimelenga kuwajengea uwezo Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria katika kutekeleza Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Amesema, anaamini mada zilizowasilishwa zimeeleka kwa vizuri na washiriki wameahidi kuzifanyia kazi mafunzo haya kwa umahiri mkubwa sana na kuhakikisha wanahimiza haki na wajibu kwa watumishi wa umma.

Ameongeza kuwa maofisa hao pamoja na mambo mengine wamepitishwa katika masuala ya maslahi ya watumishi, uzingatiaji wa maadili mahala pa kazi, mifumo ya TEHAMA Serikalini, kutambua mifumo ya upimaji wa utendaji kazi Serikalini, utaratibu wa kuendesha mashauri ya kinidhamu katika utumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati akifunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Jijini Dodoma.

Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa (katikati) akijibu hoja zilizowasilishwa na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Muundo na mgawanyiko wa majukumu wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma

Afisa Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Edwin Bilikundi akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu utaratibu wa kuendesha mashauri ya nidhamu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi yake mara baada kufunga kikao kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilichofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada ya kufunga kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.