Friday, March 8, 2024

MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. SENYAMULE ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA RAIS-UTUMISHI



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule leo Alhamisi  Machi 07,  2024 ametembelea Banda la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo katika  Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma ambako Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanayofanyika kwa muda siku tano kuanzia leo.

 

.Mhe. Senyamule pamoja na mambo mengine ameipongeza Ofisi ya Rais- UTUMISHI kwa kushiriki katika Maonesho hayo huku akiitaka itoe huduma nzuri  kwa  Watanzania ili kukidhi ndoto ya Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia Watanzania wote kwa usawa.


Tanzania inaungana na nchi nyingi Duniani katika kuadhimisha  Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka  Machi 8, 2024 kwa kuthamini na kutambua mchango wa wanawake katika ujenzi wa jamii na taifa bora kiujumla 

 





Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Salama Mohamed akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule wakati alipotembelea banda la Ofisi hiyo kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kwa muda siku tano

 


 Baadhi ya Wakurugenzi wanawake  kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakiwa kwenye picha ya pamoja  mar baada ya kutembelea banda la Ofisi hiyo kabla ya kufunguliwa kwa  Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kwa muda siku tano

 


 Baadhi ya Wakurugenzi wanawake  kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakiwa kwenye picha ya pamoja  mar baada ya kutembelea banda la Ofisi hiyo kabla ya kufunguliwa kwa  Maonesho ya Wiki ya Wanawake yanayofanyika katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kwa muda siku tano

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment