Na. Veronica Mwafisi – MADABA, RUVUMA
Tarehe 14 Machi, 2024
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewapongeza wananchi wa kijiji cha Lituta katika halmashauri ya Wilaya Madaba mkoa wa Ruvuma kwa kutoa ushirikiano hadi kujengewa Soko la Kisasa.
Mhe. Kikwete amesema kuwa mradi huo wa soko la kisasa uliombwa na wananchi wa Madaba kupitia kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt. Joseph Mhagama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.
“Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora alipokea maombi yenu na akaridhia fedha zitengwe na hatimaye kupitishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Bunge kwa jumla ili kuondoa changamoto ya soko katika Kijiji cha Lituta” ameongeza Mhe. Kikwete
Aidha, ujenzi wa Soko hili ni moja ya jitihada mahususi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwatoa wananchi katika wimbi la umaskini kwa kuwa wananchi watafanya biashara katika maeneo safi na wateja wataongezeka, hivyo kuinua uchumi wa wanamadaba.
Pia, amebainisha kuwa awali soko lilikuwa na hadhi ya chini na sasa wananchi wamepata visimba vya hali nzuri. Soko la awali lilikuwa na vizimba 34 wakati la sasa lina vizimba 80. Usanifu na ujenzi umezingatia mahitaji ya sasa na ya baadae.
Hali
kadhalika, Mhe. Dkt. Mhagama amewapongeza viongozi na watendaji wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuisimamia vizuri TASAF na
kuhakikisha jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
za kutafuta fedha na kuhudumia wananchi wake zinafanyika kwa ufanisi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa soko, vyoo na vizimba katika Kijiji cha Lituta, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.
Joseph Mhagama akisalimiana
na wananchi na walengwa wa TASAF wakati wa ziara ya kamati yake iliyolenga
kukagua utekelezaji wa mradi ya TASAF wa soko, vyoo na vizimba katika Kijiji cha
Lituta, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea.
Baadhi
ya wananchi na walengwa wa TASAF
wakimsikiliza Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.
Joseph Mhagama wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara ya kamati yake iliyolenga
kukagua utekelezaji wa mradi wa soko, vyoo na vizimba katika Kijiji cha Lituta,
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt.
Joseph Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na walengwa
wa TASAF na wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa mradi wa soko, vyoo na vizimba katika Kijiji
cha Lituta, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea.
Muonekano wa Soko linalojengwa kupitia utekelezaji
wa mradi wa TASAF katika Kijiji
cha Lituta, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea.
No comments:
Post a Comment