Na. Veronica Mwafisi - Njombe
Tarehe 13 Machi, 2024
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,
Mhe. Dkt. Joseph Mhagama kwa niaba ya Wajumbe wa kamati hiyo amefurahishwa na namna TASAF ilivyojenga jengo la kuhudumia
mama na mtoto kutokana na fedha ambazo zinatolewa na Serikali ya Rais Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Mhagama amesema kuwa
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Mama na anajali afya ya mama na mtoto mathalani
ameleta fedha nyingi na kujenga jengo ambalo ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii
ya wana Njombe na watanzania wote kwa jumla.
“Mimi pamoja na kamati yangu tumeridhika na ujenzi
wa jengo hili la kuhudumia mama na mtoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji
wa Njombe na tunaomba jengo hili litumike kama mfano kwa Halmashauri nyingine
hapa nchini” ameongeza Mhe. Mhagama.
Aidha, amefafanua kuwa ujio wao wa kukagua miradi
ya maendeleo ni maelekezo ya Kiti cha Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anakiu ya kujua iwapo fedha zinazoombwa
na Wizara na kupitishwa na Bunge kwa lengo la utekelezaji wa miradi ya
maendeleo nchini zinafika katika maeneo husika na kutatua changamoto za
wananchi.
Vilevile, Mhe.
Mhagama ameipongeza TASAF kwa kuendelea kutekeleza miradi ambayo inaacha alama
ya kudumu kwa jamii na taifa kwa jumla. Pia, kwa kufanya kazi kubwa ya kunusuru
kaya maskini katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, miundombinu ya
barabara na afya bila ubaguzi wa kiitikadi kwa wananchi.
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimeti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewasihi wana Njombe
kutambua kuwa ujauzito ni baraka kutoka kwa Mungu na sio
ugonjwa, hivyo watumie
fursa ya kukamilika kwa jengo hilo ili kupata huduma ya mama na mtoto ikiwa ni
pamoja na Watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda (Watoto njiti) na wale wenye uzito mdogo.
Pia, Mhe. Kikwete amempongeza Waziri wa
Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kuleta vifaa tiba katika
hospitali hiyo ya Halmashauri ya Mji wa Njombe ili
kuendelea kuokoa afya ya mama na mtoto.
Mhe. Kikwete ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa Njombe
kushirikiana katika utunzaji wa jengo na miundombinu yake ili iweze kunufaisha
wananchi wote.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi waliofika katika hospitali ya Mji Njombe wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika hospitali hiyo kupitia TASAF.
Baadhi
ya wananchi na walengwa wa TASAF wa halmashauri ya Mji Njombe wakimsikiliza Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt.
Joseph Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua mradi wa ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika hospitali hiyo kupitia
TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama kuzungumza
na walengwa wa TASAF na wananchi waliofika katika hospitali ya Mji Njombe wakati
kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi kukagua mradi wa ujenzi wa Wodi ya Mama
na Mtoto katika hospitali hiyo kupitia TASAF.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria wakati wakitazama miundombinu ya jengo la Wodi ya Mama na
Mtoto lililojengwa kupitia mradi wa TASAF.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati yake mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika hospitali ya Mji Njombe iliyojengwa kupitia mradi wa TASAF. Wengine ni Viongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Muonekano wa Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa
kupitia mradi wa Ujenzi wa TASAF katika hospitali ya Mji Njombe.
No comments:
Post a Comment