Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 19 Machi, 2024
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George
Simbachawene amewataka Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria kutoka katika
Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kutoa ushauri mahususi kwa
Maafisa Masuuli wao ili kuepuka kuipa hasara Serikali.
“Ninajua
kusimamia rasilimaliwatu sio jambo jepesi kwani linahitaji hekima na busara. Wapo baadhi ya Maafisa Masuuli
ambao hawasikilizi na hawapendi kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maofisa wao na hivyo kutoa uamuzi
kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo kuipa hasara Serikali”
amesema Mhe. Simbachawene.
Mhe.
Simbachawene ameongeza kuwa, iwapo sheria
na kanuni za usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma hautazingatiwa, utaondoa
adhima ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na utumishi wa umma unaotenda
haki na wenye kuwajibika kwa
umma.
Aidha, amebainisha kuwa, taasisi za
umma zinapokuwa na malalamiko
mengi ya watumishi ni ishara kuwa watendaji wa ofisi hizo hawafanyi kazi
ipasavyo hata kama lalamiko liko
ndani ya uwezo wao. Hivyo, kitendo cha kupeleka malalamiko
hayo katika ngazi za juu kwa utatuzi ni dhihaka kwa utawala.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi
amesema Maofisa hao ni washauri wakuu wa Maafisa Masuuli katika taasisi zao,
hivyo wanatakiwa kutoa ushauri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili
kuepuka kuumiza watumishi.
Bw.
Mkomi amewasihi maofisa hao kuhakikisha wanatatua matatizo ya watumishi wa umma
kwa kuwasikiliza na wakati mwingine kuwaonya kwanza kuliko kuwafukuza katika
utumishi wa umma jambo.
Awali, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria
katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Hilda Kabissa amesema kikao kazi hiki
kimelenga kuwajengea uwezo Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria katika
kutekeleza Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Amesema, anaamini mada zilizowasilishwa zimeeleka kwa
vizuri na washiriki wameahidi kuzifanyia kazi mafunzo haya kwa umahiri mkubwa
sana na kuhakikisha wanahimiza haki na wajibu kwa watumishi wa umma.
Ameongeza kuwa maofisa hao pamoja na mambo mengine
wamepitishwa katika masuala ya maslahi ya watumishi, uzingatiaji wa maadili
mahala pa kazi, mifumo ya TEHAMA Serikalini, kutambua mifumo ya upimaji wa
utendaji kazi Serikalini, utaratibu wa kuendesha mashauri ya kinidhamu katika
utumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu wakati akifunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Jijini Dodoma.
Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga
kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. George Simbachawene wakati wa kufunga kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi.
Hilda Kabissa (katikati) akijibu hoja zilizowasilishwa na Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu wakati wa kikao kazi cha
kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Uendelezaji Taasisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Bw. Nolasco Kipanda akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu Muundo na mgawanyiko
wa majukumu wakati wa
kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Afisa Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Edwin Bilikundi akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu utaratibu wa kuendesha mashauri ya nidhamu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Ofisi yake mara
baada kufunga kikao
kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na
Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada ya kufunga kikao
kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment