Sunday, March 24, 2024

KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25 YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

 


KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MWAKA 2024/25 YA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Na Lusungu Helela-Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. 

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Machi 23, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati hiyo na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.  

Amesema baada ya majadiliano mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na bajeti iliyotengwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia. 

“Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” amebainisha Mhe. Kyombo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati hiyo kwa ushauri na kupitia bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ya kuboresha kabla ya kuiwasilisha kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.

“Mimi pamoja na timu yangu, tunatoa shukrani za dhati kwa jinsi mnavyotoa michango yenu yenye muelekeo wa kuboresha Utumishi wa Umma nchini ili kukidhi matakwa  na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Simbachawene.

 

 


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25. 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao  cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kilicholenga kuwasilisha tarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini  ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25 

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Juma Mkomi  akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao  cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zilizo zote  chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka, Bw. Firmin Msiangi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha  2024/25

 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akitoa ufafanuzi wa  hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha Kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  ya kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote  zilizo chini ya Ofisi hiyo   kwa mwaka wa fedha  2024/25

 

Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao  cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Watendaji wa ofisi hiyo wakati wa  uwasilishaji wa tarifa  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zilizo zote  chini ya Ofisi kwa mwaka wa fedha  2024/25

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Mashimba Ndaki  akichangia hoja kuhusu masuala ya utumishi  wakati wa kikao  cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi  ya Taasisi zote  zilizo chini ya Ofisi hiyo  kwa mwaka wa fedha  2024/25

 


No comments:

Post a Comment