Na.Lusungu Helela- Dodoma
Tarehe 26 Machi, 2024
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Juma Mkomi amewataka Watumishi katika ofisi yake kupendana na kuthaminiana mahali pa kazi huku akiwasihi kuacha tabia ya kuhujumiana.
Ametoa kauli hiyo leo Machi 26, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichowakutanisha Watumishi hao pamoja na baadhi ya Wajumbe wa TUGHE Taifa.
"Sisi ni jicho katika Utumishi wa Umma tujitahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana ili kutimiza malengo tuliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa watumishi na wananchi kwa jumla kwa haraka na kwa ufanisi " amesisitiza Mkomi.
Bw. Mkomi amewataka watumishi hao kupendana kwa kuwa sehemu kubwa ya muda wao unatumika kazini. Hivyo, mazingira ya kazi yanatakiwa kuwa na amani na utulivu ili ufanisi uongezeke na mwananchi aweze kupata huduma bora.
Vilevile, ametoa wito kwa Wakurugenzi wote kuwaandaa watumishi walio chini yao kwa ajili ya kurithishana madaraka na kuwapa majukumu watumishi hao ili kuwajengea uwezo kiutendaji na kuwafanya waoneshe uwezo wao kazini.
Aidha, Katibu Mkuu Mkomi amewanyooshea vidole baadhi ya watumishi wenye tabia ya kuvujisha siri ambapo amewatahadharisha kuwa yeyote atakayebainika hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, TUGHE Bw.
Nsubisi Mwasandende ametumia fursa ya mkutano huo kuwaomba Wakurugenzi wa Idara
na Vitengo kuwasikiliza watumishi walio chini yao kwa kuwa wanaweza kuwa na mawazo
mazuri yenye kujenga taasisi na Serikali kwa jumla.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi yake uliolenga kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe
wa Mkutano
Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw.
Juma Mkomi (aliyekaa meza kuu) wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo uliolenga
kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025
uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Julieth
Magambo akiwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha
2024/2025 kwa Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la
Wafanyakazi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dodoma. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango, Bw. Cosmas Ngangaji akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati
wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi
hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bw. Mussa Magufuli.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya
mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 wakati wa
Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika jijini
Dodoma.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu-TUGHE, Bw. Nsubisi Mwasandende akiwasilisha hoja kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo
uliofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Mkutano
Maalum wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Shaha Nampeha akichangia moja ya hoja
wakati wa mkutano huo uliolenga kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya bajeti na
mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia wasilisho la taarifa ya mapendekezo ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa
katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi wa
Ofisi yake mara baada ya kufungua mkutano huo uliolenga kuwasilisha mapendekezo
ya bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment