Na Lusungu Helela-Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Ofisi
yake kutoa huduma bora kwa wananchi kwa haraka na ufanisi, huku akisisitiza
ubora wa huduma hizo uendane na uzuri wa jengo jipya ambalo Ofisi hiyo imehamia
hivi karibuni.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jana jioni mara baada ya
Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo na kuwakutanisha Watumishi wote wa Ofisi hiyo
wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,
ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia
katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba
Jijini Dodoma.
Amesema anatamani kuona wananchi na watumishi wanaohudumiwa
katika jengo hilo jipya wanafurahia huduma wanazozipata kwani kitendo cha
Watumishi kuhamia katika jengo hilo jipya kwa sasa kuna utulivu wa akili.
“Sasa watumishi wote tupo katika jengo moja, sitegemei kusikia
visingizio vya hapa na pale kuwa jalada fulani halipo Mtumba bali liko
Ofisi za UDOM kule ambako baadhi ya watumishi walikuwa wakifanya kazi, tufanye
kazi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Amesema kitendo cha Watumishi kuhamia katika jengo moja tofauti
na ilivyokuwa mwanzo ni muhimu sasa kwa Watumishi wa Ofisi yake kushirikiana
katika kufanya kazi ili kuhakikisha wateja wanaridhika na huduma wanazozipata.
"Serikali imejenga jengo zuri mno, hii kwenu ni motisha kubwa,
hivyo hakikisheni huduma mnazozitoa ziwe za viwango vya hali ya juu ili
kuendana na thamani ya jengo" amesema Mhe. Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene ameiagiza Ofisi hiyo kuweka utaratibu
wa kufanya mazoezi kwa pamoja lengo likiwa ni kulinda afya pamoja na kujikinga
na magonjwa yasiyoambukiza ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
"Kwa sasa tupo jengo moja, naagiza utaratibu uandaliwe wa
kufanya mazoezi kwa pamoja ili kulinda afya zetu na kuwahudumia wananchi
ipasavyo" amesema Mhe.Simbachawene
Awali, Katibu Mkuu UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi alimshukuru Waziri
Simbachawene kwa wazo la kuandaa Iftar hiyo huku akiwataka Watumishi wa Ofisi
yake kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.
"Mtaungana nami, leo ni siku muhimu sana ambapo Waislamu
mpo katika mfungo wa Ramadhani huku Wakristo mkiwa katika mfungo wa Kwaresma,
tumekutana hapa ili kufuturu pamoja kuonyesha ishara ya upendo na ushirikiano,"
Bw. Mkomi amesisitiza.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi
akitoa neno la shukrani kwa Waziri Simbachawene amemuahidi kuwa maagizo
yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu ikiwemo
utamaduni wa namna hiyo wa kukutana kwa pamoja.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa
katika mstari wakichukua futari jana jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na
Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote
walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akizungumza jana jioni na
Watumishi wa Ofisi yake kabla ya Iftar
iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi
wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akitoa neneo la shukrani kwa jana jioni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mbele ya Watumishi
wa Ofisi hiyo baada ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wakimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi
hiyo ambapo Watumishi wote
walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
(katikati) akiwa na Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Xavier
Daudi ( kushoto) wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Baadhi ya Maafisa wa Ofisi
ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa katika mstari wakichukua futari jana
jioni wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wakiwa katika Iftar
iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi
wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya
viongozi kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu
ya kujumuika kwa pamoja mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo
Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa
na nyuso za furaha jana jioni mara baada
ya Iftar iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ambapo Watumishi wote walikutanishwa wakiwemo baadhi ya viongozi kutoka Taasisi
zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujumuika kwa pamoja
mara baada ya kuhamia katika jengo jipya lililopo Mtaa wa Utumishi, Mji
wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment