Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 18 Machi, 2024
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.
Xavier Daudi amewataka Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kutambua kuwa
kada zao ni za kimkakati kwa maendeleo ya Taifa.
“Rasilimaliwatu
na Sheria vikisimamiwa vibaya vinaweza kuleta matokeo hasi katika utendaji kazi
hivyo, kushusha uchumi na kusababisha taifa kushindwa kufikia malengo yake ya
kutoa huduma bora kwa umma” amesisitiza Bw. Daudi.
Bw.
Daudi ameyasema hayo leo tarehe 18 Machi, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi
wa Umma.
Ameongeza
kuwa Sheria, Kanuni na Miongozo inayotumika sasa imetengenezwa na viongozi
waliotangulia ambao walitamani kuona utumishi wa umma nchini unaendelea, hivyo
Maafisa hao wametakiwa kuongeza ubunifu na kutenda haki katika utekelezaji
wake.
Aidha Bw.
Daudi amesema uzembe na kutokuwa na tabia ya kujisomea kumesababisha kuwa na
changamoto ya ukiukwaji wa sheria, kanuni, miongozo ya kazi katika utumishi wa
umma.
Akitoa
neno la utangulizi, Mkurugenzi wa
Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa ameelezea lengo la kikao
kazi hicho kuwa ni kukumbushana kuhusu namna bora ya kutekeleza Sheria za Utumishi
wa Umma na kanuni zake na kubadilishana uzoefu.
Bi. Hilda amebainisha
kuwa, baadhi ya maafisa wa taasisi za umma wamekuwa wakiandika barua kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiomba ufafanuzi wa
masuala ya kawaida na ambayo yangeweza kutatuliwa katika maeneo yao kwa haraka,
hivyo kikao hiki kitawajenga na kuwapa uelewa wa pamoja na namna bora ya
kushughulikia masuala hayo ya kiutumishi mahala pa kazi.
Kikao
kazi hicho kinafanyika kwa muda wa siku mbili tarehe 18 na 19 Machi, 2024
katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza
na Maafisa
Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi alipokuwa
akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Bi.
Hilda Kabissa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu,
Bw. Xavier Daudi kufungua kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa
Umma, Bi Felista Shuli akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa
Rasilimaliwatu kuhusu ushughulikiaji wa uhamisho (e-transfer), upandishwaji
vyeo na ubadilishaji kada wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa
Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, SACP. Ibrahim Mahumi akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na
Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu ushughulikiaji wa malimbikizo ya mishahara wakati
wa kikao
kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu uzingatiwaji wa maadili mahala pa kazi wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Mkurugenzi Msaidizi wa Mishahara, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Gubas Vyagusa akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu kuhusu ushughulikiaji wa maslahi ya watumishi wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Afisa Sheria, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Bi. Amina Natepe akiwasilisha mada kwa Maafisa Sheria na Maafisa
Rasilimaliwatu kuhusu mambo ya muhimu ya kuzingatia katika Sheria ya Utumishi
wa Umma na Kanuni zake wakati wa kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiwa
katika picha ya pamoja na Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu mara baada
ya Kaimu Katibu Mkuu huyo kufungua kikao kazi cha kujadili changamoto za utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment