Friday, October 27, 2023

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAIDHINISHA VIBALI 930 VYA AJIRA MPYA KWA KADA YA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2023/24

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 27 Oktoba, 2023

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeidhinisha jumla ya nafasi 930 za ajira mpya za kada ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka katika mwaka wa fedha 2023/24 na kutoa nafasi 443 za ajira mpya kwa kada hiyo katika mwaka wa fedha 2022/23.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano Mkuu wa 11 wa wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) jijini Dodoma.

Mhe. Simbachawene amesema, uidhinishaji wa vibali hivyo vya ajira mpya unaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kwa ustawi wa taifa.

Ameongeza kuwa, kwa kutambua mchango wa kada hii katika ustawi wa Utumishi wa Umma, jumla ya Watunza Kumbukumbu 649 waliokasimiwa katika Ikama na Bajeti ya mwaka 2022/23 wameshapandishwa vyeo na kuidhinishiwa mishahara ya vyeo vipya mwezi Juni, 2023. 

Katika kushughulikia changamoto za kiutumishi kwa kada hii ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka, Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora imekamilisha zoezi la kuhuisha Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Kada ya Watunza Kumbukubu na Nyaraka na Muundo ambao ulianza kutumika kuanzia tarehe 01 Julai, 2023.

Ili kuongeza ari na morali ya utekelezaji wa majukumu ya watumishi wa umma, Mhe. Simbachawene amesema Serikali itaendelea kupandisha vyeo Kada hii na Watumishi wa Umma wengine kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mhe. Simbachawene amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi wa TRAMPA na kusimamia utendaji kazi wa Wataalam wa kada hii  pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kisera na kiutendaji ili kuwezesha utoaji wa huduma bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.

Mkutano wa wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) hufanyika kila mwaka ambapo wataalam hawa hupata muda wa kujikumbusha masuala mbalimbali yanayohusiana na taaluma yao na mafunzo mbalimbali kuhusu Maadili ya Utendaji kazi, Miundo ya Maendeleo ya Utumishi iliyopo Serikalini ikiwemo kada yao, Uendeshaji wa Serikali, Usalama na Utunzaji Siri za Serikali.  

Mkutano huu wa siku tatu unafanyika kwa kaulimbiu isemayo“Utunzaji bora wa Kumbukumbu na Nyaraka ni Chachu ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa”

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) uliofanyika jijini Dodoma.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akitoa maelezo ya awali kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu mkutano wa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) uliofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Dodoma.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akipokea zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) wakati wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama hicho uliofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene aliyekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya chama hicho.





 

 

 

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TRAMPA JIJINI DODOMA

 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora   mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kukagua maandalizi ya mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka unaotarajiwa  kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,  Jijini Dodoma.


Baadhi ya  Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka wakimsiliza  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kukagua maandalizi ya mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka  ambapo Mgeni Rasmi wa Mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tnzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma, Bw. Xavier Daudi  akizungumza kabla ya kumkaribisha  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kukagua maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka unaotarajiwa  kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,  Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka mara baada ya kuwasili kwa ajili ya  kukagua maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka hao unaotarajiwa  kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,  Jijini Dodoma.





Thursday, October 26, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA,KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

1.    Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ) kwa mwaka 2022/23



1.    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kilicholenga kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Abeid Ramadhan akichangia hoja kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ) kwa mwaka 2022/23.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Alice Kaijage akichangia hoja kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ) kwa mwaka 2022/23.


Tuesday, October 24, 2023

OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE ZAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  kilicholenga kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.

Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akijibu moja ya hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho akitoa ufafanuzi wa hoja za masuala ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Innocent Bomani akijibu moja ya hoja ya masuala ya ajira kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Jonas Zeeland (Aliyenyanyua mkono) akichangia hoja kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.


Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Watendaji wa ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.




Thursday, October 19, 2023

WARATIBU WA TASAF HANDENI WAPONGEZWA KWA KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WAO KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA TASAF

Na. Rainer Budodi- Handeni

Tarehe 19 Oktoba, 2023

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa kuwashirikisha viongozi wao juu ya matumizi ya fedha za miradi ya TASAF inayopelekwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa maendeleo ya miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

“Nawapongeza sana Waratibu wa Halmashauri hii ya Handeni kwa kuwashirikisha viongozi wenu katika matumizi ya fedha zinazoletwa na TASAF, ushirikiano huu ni mzuri kwa sababu fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa uwazi bila kificho chochote ili kutimiza malengo yaliyokusudia,” Mhe. Simbachawene ameongeza. 

Amesema viongozi wengi katika Halmashauri za Wilaya hawana taarifa juu ya fedha za miradi ya TASAF zinazoingia katika Wilaya zao lakini imekuwa tofauti kwa Wilaya ya Handeni, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo katika maelezo yake anaonekana kuufahamu vizuri utekelezaji wa mradi huu. 

“Mkuu wa Wilaya, nimefurahi sana kuona kuwa mradi huu unauelewa vizuri maana umeuzungumzia vizuri sana, hii inaonyesha kuwa unashirikishwa kikamilifu, na hivi ndivyo inavyotakiwa,” Mhe. Simbachawene ameongeza. 

Amemsisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo ya Handeni Mhe. Albert Msando kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kuwaachia waratibu pekee kwa kuwa fedha za miradi zinazopelekwa ni nyingi, hivyo zinahitaji usimamizi ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa. 

Mhe. Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ya kuzungumza na watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri za Wilaya ya Mkinga, Korogwe na Handeni mkoani Tanga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikata utepe kuzindua mradi wa kivuko uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando kuhusu mradi wa kivuko uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo. 


Sehemu ya wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiangalia bango linaloonyesha miradi inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akionyesha kutaka ufafanuzi wa moja ya mradi ulioko kwenye bango linaloonyesha miradi inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.