Thursday, October 19, 2023

WARATIBU WA TASAF HANDENI WAPONGEZWA KWA KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WAO KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA TASAF

Na. Rainer Budodi- Handeni

Tarehe 19 Oktoba, 2023

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa kuwashirikisha viongozi wao juu ya matumizi ya fedha za miradi ya TASAF inayopelekwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa maendeleo ya miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

“Nawapongeza sana Waratibu wa Halmashauri hii ya Handeni kwa kuwashirikisha viongozi wenu katika matumizi ya fedha zinazoletwa na TASAF, ushirikiano huu ni mzuri kwa sababu fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa uwazi bila kificho chochote ili kutimiza malengo yaliyokusudia,” Mhe. Simbachawene ameongeza. 

Amesema viongozi wengi katika Halmashauri za Wilaya hawana taarifa juu ya fedha za miradi ya TASAF zinazoingia katika Wilaya zao lakini imekuwa tofauti kwa Wilaya ya Handeni, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo katika maelezo yake anaonekana kuufahamu vizuri utekelezaji wa mradi huu. 

“Mkuu wa Wilaya, nimefurahi sana kuona kuwa mradi huu unauelewa vizuri maana umeuzungumzia vizuri sana, hii inaonyesha kuwa unashirikishwa kikamilifu, na hivi ndivyo inavyotakiwa,” Mhe. Simbachawene ameongeza. 

Amemsisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo ya Handeni Mhe. Albert Msando kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kuwaachia waratibu pekee kwa kuwa fedha za miradi zinazopelekwa ni nyingi, hivyo zinahitaji usimamizi ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa. 

Mhe. Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ya kuzungumza na watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri za Wilaya ya Mkinga, Korogwe na Handeni mkoani Tanga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikata utepe kuzindua mradi wa kivuko uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando kuhusu mradi wa kivuko uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo. 


Sehemu ya wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiangalia bango linaloonyesha miradi inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akionyesha kutaka ufafanuzi wa moja ya mradi ulioko kwenye bango linaloonyesha miradi inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga. 


 

No comments:

Post a Comment