Wednesday, October 18, 2023

WATUMISHI WACHAPAKAZI WATAMBULIWE - Mhe. Simbachawene

Na. Rainer Budodi- Korogwe

Tarehe 18 Oktoba, 2023

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa Waajiri na Maafisa Utumishi katika taasisi za umma kuwatambua watumishi wenye uwezo kiutendaji ili wapate motisha ya kuendelea kuchapa kazi na kuwafungulia milango ya kupanda vyeo.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kusikiliza changamoto za watumishi na kuzifanyia kazi.

“Nimefurahi sana kumsikia Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kalisti Lazaro akimzungumzia vizuri mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe juu ya utendaji kazi wake, na ninyi Watendaji na Maafisa Utumishi muwasemee vizuri watumishi wanaofanya kazi kwa bidii, kwa kuwa ninyi ndio mnaowafahamu watumishi wenu” ameongeza Mhe. Simbachawene.

Aidha, Mhe. Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iko wazi na imetoa uhuru wa kuongea na wao wakiwa ndio wasaidizi, wanamsaidia kwa kufanya ziara maeneo mbalimbali nchini ili kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuzifanyia kazi kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Sisi tupo kumsaidia Rais wetu mpendwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo mtoe dukuku zenu, maoni na pongezi ili kuboresha utumishi wa umma kwa lengo la kuwahudumia wananchi ipasavyo” Mhe. Simbachawene.

Ameongeza kuwa, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi mazuri kwa watumishi wa umma ikiwemo kulipa madeni, kupandisha vyeo na stahiki nyingine mbalimbali, hivyo watumishi wana deni la kulipa kwa kuchapa kazi kwa bidii katika kuwatumikia watanzania.




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiandika hoja za watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika kikao kazi chake na watumishi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kalisti Lazaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifafanua hoja za watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika kikao kazi chake na watumishi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kalisti Lazaro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisikiliza hoja za watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika kikao kazi chake na watumishi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe. Kalisti Lazaro.


Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika kikao kazi chake na watumishi hao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.


Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.


Dkt. Miriam Cheche wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Mkoa wa Tanga.


Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Bw. Juma Swedi akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Mkoa wa Tanga.


 

No comments:

Post a Comment