Tarehe 11 Oktoba, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka Wakuu wa Idara na
Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kushirikiana
na Wakuu wa Taasisi zao
kuhakikisha watumishi wa Umma wanapata haki zao za kiutumishi kwa wakati bila kuhangaishwa ili waweze kutulia katika vituo
vyao vya kazi na kutekeleza kikamilifu majukumu yao ya utoaji wa huduma kwa
wananchi.
“Ninawapongeza waajiri wote wanaowalinda watumishi wao
ili rasilimali hiyo iweze kufanya kazi kwa ukamilifu na ufanisi, kwani bila hao
hakuna chochote kitakachoweza kufanyika,” Mhe. Simbachawene amesisitiza na
kutoa rai kwa wakuu hao kuzingatia misingi ya Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na
Miongozo mbalimbali katika Utumishi wa Umma na kuhakikisha watumishi wa Umma
walio katika Taasisi zao wanatekeleza wajibu wao ipasavyo ili Serikali iweze
kupata tija ya uwepo wao.
Mhe. Simbachawene amesema Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu ndio wasimamizi wa watumishi hivyo wasipowasaidia
katika kutatua changamoto zao za kiutumishi ni sawa na uhujumu uchumi.
Ametoa siku 14 kuanzia leo kwa Wakuu wa Idara hizo
kufanyia kazi changamoto za kiutumishi yakiwemo madai ya malipo mbalimbali ya
watumishi na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI na taarifa ya jinsi
walivyoshughulikia changamoto hizo.
“Katibu Mkuu, natoa siku 14 kuanzia leo, tupate
taarifa ya namna madai ya malipo mbalimbali ya watumishi yalivyoshughulikiwa
kwani tunatakiwa tutatue changamoto za watumishi hawa ili wawahudumie wananchi
kwa furaha,” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Pia, amesisitiza kuhusu uzingatiaji wa maadili
kwa kuwa ofisi yake imeendelea
kupokea malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo rushwa, lugha zisizofaa,
kufanya udanganyifu wa nyaraka ikiwemo kughushi barua za masuala mbalimbali ya
kiutumishi kama uhamisho wa kwenda sehemu zenye maslahi mazuri. Hivyo, ametoa wito kwa watumishi wote wanaojihusisha
na tabia hiyo kuacha mara moja na hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa
wahusika.
Vilevile,
aliwaekeleza baadhi ya Waajiri kuacha tabia ya kukataa kuwapokea watumishi
wanaohamishiwa kwenye taasisi zao na baadhi kutoruhusu watumishi kuhama hata
pale inapoelekezwa na Mamlaka. “Suala hili ni kinyume na sheria, kanuni na
taratibu kwa kuwa kitendo hicho ni kukosa utii kwa Serikali pamoja na Mamlaka
zilizo juu yao,” Amesisitiza
Akitoa
maelezo ya awali kuhusu lengo la kikao kazi hicho, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amesema kikao hicho kinajadili
changamoto zinazoendana na utekelezaji wa majukumu ya utawala na usimamizi wa
rasilimaliwatu na namna bora ya kukabiliana nazo.
Ameongeza
kuwa, washiriki watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kuelimishana kuhusu
taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kushughulikia masuala mbalimbali ya
utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma ili kuimarisha
na kuboresha utendaji kazi kwa madhumuni ya kutoa huduma zenye tija kwa taifa
na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa kiwango kinachotarajiwa.
Kikao
kazi hicho cha siku tatu kimeandaliwa mahususi kwa lengo la kutathmini nafasi
ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala katika kuwezesha utendaji wa taasisi
na utumishi wa umma kwa jumla.
Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma na watendaji wengine wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati akifungua kikao kazi cha wakuu
hao leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier
Daudi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Arusha (AICC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Idara za Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati akifungua kikao
kazi cha wakuu hao leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Arusha (AICC).
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika
kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano Arusha (AICC).
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika
kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano Arusha (AICC).
Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na watendaji wa serikali
wakiwa katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe 11/10/2023 katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa
Umma, Bi. Felister Shuli akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa
Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
kilichoanza leo tarehe 11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda
akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe
11/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akiwasilisha mada
wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe 11/10/2023 katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa tuzo ya usimamizi bora wa
rasilimaliwatu kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Tanga Jiji, Bi.
Mwanaidi Nondo mara baada ya jiji hilo kushika nafasi ya tatu kwa upande wa
majiji wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa
Rasilimawaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo tarehe 11/10/2023
katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
No comments:
Post a Comment