Na. Rainer Budodi- Dar es
Salaam
Tarehe 16 Oktoba, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa Waajiri wote katika taasisi za umma kusoma, kuelewa na kutumia kikamilifu Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia na kuzingatia masuala ya Jinsia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema
hayo wakati wa tukio la uzinduzi wa
Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma na Ufunguzi wa
Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne yanayoendeshwa na Taasisi ya UONGOZI
kwa kushirikiana na Serikali ya Finland leo tarehe 16 Oktoba, 2023 katika
ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Mhe. Simbachawene ameilekeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kusambaza mwongozo huo kwenye mamlaka zote za ajira katika Utumishi wa Umma na kushirikiana na Mamlaka hizo kuendesha mafunzo ili kuimarisha usawa na hatimaye kuondoa aina zote za ubaguzi mahali pa kazi.
“Ninawaelekeza waajiri wote katika taasisi za umma kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza afua za usimamizi wa masuala ya jinsia mahala pa kazi na kutenga bajeti kwa kila mwaka wa fedha ili kumuwezesha Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Taasisi husika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na uratibu wa mafunzo ya Jinsia katika Utumishi wa Umma kwenye Taasisi husika” alisisitiza Mhe. Simbachawene.
Vilevile, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI kushirikiana na Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuzifikia Mamlaka zote za Mikoa 26 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 ili kutoa mafunzo kuhusu Mwongozo huo ili kila mtumishi wa umma apate uelewa wa kutosha na kuepuka kuwa na ubaguzi mahali pa kazi.
Vile
vile, Mhe. Simbachawene amefafanua kuwa ili Taifa liweze kufikia usawa wa
kijinsia, hasa kwenye masuala ya uongozi, hakuna budi kushirikisha wanaume
katika utekelezaji wa mipango na jitihada mbalimbali za kufanikisha azma za
wanawake kuwa viongozi.
“Kila
mmoja anaona kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan ni kinara na mfano wa kuigwa katika kuinua wanawake na ameendelea
kujipambanua katika uimarishaji wa haki na uwezeshaji wa wanawake kwa kuwateua
na kuwapatia nafasi za uongozi.
Amesema
amefurahi kuona wanaume pia wamealikwa kwenye kongamano hilo na baadhi ya
wakufunzi kwenye programu hiyo ni wanaume.
Hivyo, ameitaka Taasisi ya UONGOZI kuendelea kuwashirikisha na kuwahusisha
kikamilifu wanaume kwenye programu hii ili kuleta matokeo yenye tija.
Mhe.
Simbachawene alihitimisha hotuba yake kwa kutoa shukrani za dhati kwa wadau wa
maendeleo wakiwemo Serikali ya Finland, Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la
Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) kwa kuendelea kuiwezesha Taasisi ya
UONGOZI kifedha na kiutaalamu (Financial and Technical Support) katika kutimiza
majukumu yake kuwajengea uwezo viongozi hususan wanawake.
Naye, Katibu Mkuu –
UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Mwongozo huo unalenga kuweka mazingira bora na
wezeshi ya ujumuishwaji wa jinsia katika Utumishi wa Umma ili kuongeza tija
katika utendaji kazi na kuimarisha masuala ya haki na usawa kati ya Wanaume na
wanawake kwa ngazi zote katika Utumishi wa Umma.
“Kupitia mwongozo huo, tunataka kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika nafasi za Uongozi na maamuzi ikiwa ni kipaumbele cha Serikali kuendeleza wanawake na kuwajengea uwezo na kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao” ameongeza.
Bw. Mkomi amebainisha
kuwa, azma ya Serikali kupitia lengo namba tano (5) la Malengo ya Maendeleo
Endelevu ya Mwaka 2030 kuhusu kufikia Usawa wa Kijinsia asilimia 50 katika
uongozi, hivyo pamoja na jitihada za Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa
Umma ambazo zimeendelea kufanywa na Serikali, bado baadhi ya Taasisi za Umma
hazijaweza kujumuisha kikamilifu masuala ya Jinsia katika mipango na bajeti za
Taasisi husika.
Ameongeza kuwa, uandaaji wa Mwongozo huo umepita awamu zote muhimu na kushirikisha kikamilifu wadau mbalimbali ikiwemo Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara zote ambao walitoa maoni yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizindua Mwongozo wa
Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma leo tarehe 16 Oktoba, 2023
katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wadau
walioshiriki tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika
Utumishi wa Umma na Ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne leo
tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene kuzindua Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi
wa Umma na kufungua Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne leo tarehe 16
Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitazama video fupi kuhusu uendeshaji wa Mafunzo ya Wanawake kabla ya kuzindua Mwongozo wa
Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma na kufungua Mafunzo ya Wanawake
Awamu ya Tatu na Nne leo tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya
Hyatt Regency Jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Dkt.
Kadari Singo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifuatilia wasilisho kuhusu
uendeshaji wa Mafunzo ya Wanawake kabla ya kuzindua Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika
Utumishi wa Umma na Ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne leo
tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akigawa nakala ya Mwongozo wa Ujumuishwaji
wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Taasisi
ya UONGOZI, Bw. Deogratias Usangira mara baada ya kuzindua Mwongozo huo leo
tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akigawa nakala ya Mwongozo wa Ujumuishwaji
wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.
Chiku Kiguhe mara baada ya kuzindua Mwongozo huo leo tarehe 16 Oktoba, 2023
katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akigawa nakala ya Mwongozo wa Ujumuishwaji
wa Jinsia katika Utumishi wa Umma kwa Bi. Ann-Cristine Nora Kafanabo Mwakilishi
wa Bi. Joyce Kafanabo Mtaalam Mwelekezi Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia
Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuzindua Mwongozo huo leo
tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam.
Sehemu ya watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na wadau
walioshiriki tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika
Utumishi wa Umma na Ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya uzinduzi
huo leo tarehe 16
Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya wadau walioshiriki tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa
Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma na Ufunguzi wa Mafunzo ya
Wanawake Awamu ya Tatu na Nne wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya uzinduzi huo leo tarehe 16
Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wadau wa
maendeleo mara baada ya kuzindua Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia katika
Utumishi wa Umma na kufungua Mafunzo ya Wanawake Awamu ya Tatu na Nne leo
tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya kuzindua Mwongozo wa
Ujumuishwaji wa Jinsia katika Utumishi wa Umma na kufungua Mafunzo ya Wanawake
Awamu ya Tatu na Nne leo tarehe 16 Oktoba, 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya
Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment