Na. Rainer Budodi-
Mkinga-Tanga
Tarehe 18 Oktoba,
2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameeleza kuwa
dhamira ya Serikali kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika ajira za muda sio
kutengeneza barabara kwa mikono bali ni kuwawekea mazingira ya kuwa na ajira
itakayowawezesha kupata kipato na kuweza kujitegemea katika kufanya kazi na
kujikomboa na wimbi la umaskini.
Mhe. Simbachawene amesema hayo wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi
ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Amesema wananchi
wamekuwa wakifanya kazi za miradi mbalimbali ya TASAF ikiwemo ujenzi wa miundombinu katika
maeneo yao akitolea mfano ujenzi wa barabara na kulipwa ujira ili waweze kujikomboa na wimbi la umasikini.
Mhe. Simbachawene ameainisha wanufaika wanaolengwa katika ajira za muda za TASAF kuwa ni wale ambao
wanakidhi masharti ya umri ambao si chini ya miaka 18 na si zaidi ya miaka 65.
Vilevile asiwe mgonjwa na asilazimishwe kufanya kazi kinyume na vigezo hivyo.
Aidha, amewasisitiza Viongozi wa
Serikali kusimamia masharti hayo ili kuepuka wasioweza kufanya kazi hizo
kulingana na vigezo vilivyowekwa wasifanye kwa kuwa hiyo sio njia pekee ambayo
walengwa wanatakiwa kuwezeshwa na TASAF lakini amewataka vijana wenye uwezo
katika kaya kutumia fursa hiyo ya ajira kwa lengo la kuzikomboa kaya zao katika
wimbi la umaskini.
“Mkinga ni miongoni mwa Wilaya za mfano kwa utekelezaji
na usimamizi mzuri wa miradi ya TASAF, ninaona na nimeridhishwa na maonesho ya shughuli zinazofanywa
na akina mama ili kujikomboa na umaskini na hatua kubwa iliyopigwa katika utelekezaji wa shughuli zenye lengo la kuondoa umasikini na kurahisisha upatikanaji
wa huduma za kijamii,” alisema.
Mhe. Simbachawene ametumia fursa ya mkutano huo kuwaomba
wananchi kufanya dua na sala kumuombea hekima, kheri na baraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa na moyo wa upendo kwa kuwa ndiye anayetafuta fedha kutoka nje na ndani ya nchi kwa lengo
la kuwakomboa wananchi wake kutoka katika wimbi la umasikini.
Awali, akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya TASAF, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Kanali
Maulid Surumbu amesema TASAF kupitia wananchi imetengeneza na kujenga barabara,
shule na zahanati ambazo zinawasaidia kwa namna moja ama nyingine kujikomboa na
wimbi la umasikini katika wilaya ya yao.
Ameongeza kuwa, wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga katika vijiji vyote wananufaika vyema na uwepo wa TASAF kwa kiwango kikubwa kwa kuwa kaya masikini zimefikiwa na zinawezeshwa kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akionja moja ya
bidhaa zinazozalishwa na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Bamba Kata ya Doda
Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiangalia moja ya
bidhaa zinazozalishwa na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Bamba Kata ya Doda
Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo ya

Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na walengwa
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) katika Kijiji cha Bamba, Kata ya Doda, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo
kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Bamba, Kata ya Doda, Wilaya ya Mkinga
mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF mkoani humo.
No comments:
Post a Comment