Na. Rainer Budodi-Mkinga-Tanga
Tarehe 17 Oktoba, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewasisitiza waajiri katika
taasisi za umma kutenga muda wa kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi
na kuzifanyia kazi kwa lengo la kuwapa ari ya kuendelea kuwahudumia wananchi
kikamilifu.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Mkoa wa
Tanga na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga, Mhe.
Simbachawene amesema rasilimaliwatu ni rasilimali muhimu sana kuliko rasilimali
nyingine yoyote katika kuleta maendeleo, hivyo wasipotatuliwa changamoto zao
hakutakuwa na matokeo chanya.
“Utatuzi wa changamoto uwe ni ajenda ya kila siku,
Viongozi wa ngazi za juu, RAS, DAS mpange ratiba ya kuwasikiliza watumishi na
kujua changamoto walizo nazo na kuangalia namna bora ya kuzitatua. Iwapo mtafanya
ziara za kuwasikiliza watumishi, ninaamini changamoto zitapungua na watumishi
watatekeleza majukumu yao kikamilifu.” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Ameongeza kuwa, yeye pamoja na viongozi wengine wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wako tayari
kushirikiana na Viongozi na Watendaji hao kutatua changamoto za watumishi na
ndio maana wamekuwa wakifanya ziara za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali
nchini ili kusikiliza changamoto za watumishi hao na kuzitatua.
“Sisi viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tuko tayari kutoa ushirikiano katika kutatua
changamoto za watumishi, kwa hiyo kaeni na watumishi wenu ili mjue changamoto
wanazokutana nazo na mzitatue, na zile zitakazohitaji ushiriki wetu msisite
kutushirikisha ili tuzitatue kwa pamoja kwa lengo la kuwafanya watumishi hawa
waweze kutoa huduma bora kwa wananchi” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewataka watumishi wa umma
kufahamu kuwa utumishi wa umma unaendeshwa kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni,Taratibu na Miongozo, hivyo ni lazima watumishi watambue taratibu hizo wanapodai
haki zao.
Amesema kuna changamoto mbalimbali zinazosababishwa na
uzembe wa watendaji na nyingine watumishi kukosa uelewa wa taratibu za kiutumishi.
Hivyo, ametoa rai kwa watumishi kusoma nyaraka za kiutumishi ili kujua wajibu na
haki za watumishi.
Mhe. Simbachawene ameanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga ya kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo kwa lengo la kuzitatua pamoja na kukagua utekezaji wa miradi ya TASAF ambapo leo ameanza na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Mkoa
wa Tanga (hawapo pichani) Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake
ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri wa
Afya, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu akitoa
shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kwa kufanya ziara katika mkoa huo kwa
lengo la kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa
mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba akitoa salamu za mkoa wake kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene wakati Waziri huyo alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo akiwa
kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene na Waziri wa Afya, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini,
Mhe Ummy Mwalimu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba
alipokuwa akitoa salamu za mkoa wake wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe.
Simbachawene mkoani Tanga iliyolenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi
ya TASAF.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
ya Mkinga alipowasili katika Wilaya hiyo kwa ziara ya kikazi iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa
mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Kanali
Maulidi Surumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Bi.
Zahara Msangi wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mkinga kilicholenga kuhimiza uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa umma wa mkoa huo na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF.
No comments:
Post a Comment