Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora akiendelea na ziara
yake ya kikazi iliyolenga kukagua,
kuzindua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
kusikiliza changamoto za wananchi katika Mkoa huo.
Thursday, July 9, 2026
MHE. KIKWETE AWASILI WILAYA YA SIKONGE MKOANI TABORA, AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KIKAZI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
TASAF AWAMU YA III YAJA, VIONGOZI ZINGATIENI VIGEZO VYA KUWAPATA WALENGWA KUEPUSHA MALALAMIKO YALIYOJITOKEZA AWAMU ZILIZOPITA - Mhe. Ridhiwani
Na. Veronica Mwafisi-Manispaa ya Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Viongozi
mkoani Tabora kuzingatia vigezo vya kuwapata walengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mhe. Kikwete amesema moja ya jambo kubwa
ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akilisisitiza ni kusaidia
Watanzania walio wanyonge. “TASAF awamu zilizopita illishia mwaka jana mwezi wa
9 lakini kwa upendo wake amepambana kuhakikisha fedha zinapatikana ili kusaidia
Watanzania hao kuepukana na umaskini,” Mhe. Kikwete ameongeza.
Akizungumza na Wananchi katika Manispaa ya
Tabora tarehe 9 Julai, 2026, baada ya kuhitimisha ziara yake kwa siku ya leo
aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya
Tabora na Manispaa ya Tabora ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,
Mhe. Ridhiwani amesema sio sawa fedha hizo zikatumika kinyume kwa kuwaingiza
kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watu wasiostahili. “Niwaombe mliopewa
dhamana ya kusimamia zoezi hili kutenda haki kwa kuwaweka walengwa stahiki,”
Mhe. Kikwete ameongeza.
Amesema kuna baadhi ya maeneo yalilalamikiwa
kwa kufanya mambo ya ajabu na kutowatendea haki walengwa katika fedha
walizokuwa wakipewa, niwaombe sana, tunapoanza mpango unaokuja, nisingependa
yale mapungufu yaliyojitokeza kipindi cha nyuma yajirudie.
Ametoa wito kwa Wananchi kushiriki katika
mikutano ya kutambua walengwa ili wapatikane watu sahihi. “Wananchi nanyi kwa
kuwa mnashiriki katika mikutano ya kuibua walengwa, mkisomewa majina ya
walengwa kama kuna ambao wameachwa mseme ili waongezwe na kama wamewekwa
wasiostahili pia mseme ili watolewe kwani mkikaa kimya ndio matokeo yake
wanaingizwa wasiostahili na baadae kuleta malalamiko.” ameongeza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa
ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia
jambo na Mjasiriamali wakati Waziri huyo
alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Wazee wa Manispaa ya Tabora wakati Waziri huyo
alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya
ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akicheza nyimbo ya ukaribisho katika
Manispaa ya Tabora alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wednesday, July 8, 2026
SIMAMIENI KIKAMILIFU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ILI THAMANI YA FEDHA IONEKANE-“Mhe. Ridhiwani
Na. Veronica Mwafisi-Sikonge na Tabora
Tarehe 09 Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameisihi Kamati ya
Miradi ya Maendeleo mkoani Tabora kusimamia kwa umakini miradi inayotekelezwa
katika maeneo mbalimbali mkoani humo ili iendane na thamani halisi ya fedha.
Mhe. Kikwete amesema hayo kwa nyakati tofauti
leo tarehe 9 Julai, 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri
ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora wakati akikagua na kuweka jiwe la
msingi na kuzindua utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Tabora.
Amesema katika kuhakikisha nchi inakuwa na
maendeleo kwenye sekta zote, Serikali itaendelea kutoa fedha za miradi ya
maendeleo, hivyo ni jukumu la wasimamizi kusimamia kwa ufasaha ili miradi hiyo
itekelezwe kikamilifu kulingana na fedha inayotolewa.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la
msingi katika kituo cha afya cha Igigwa, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.
Kikwete amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho na kusema
Serikali inahitaji eneo kubwa ili kujenga majengo mengi zaidi kwa lengo la kuwa
na huduma mbalimbali za afya.
“Kituo hiki cha afya ni kwa ajili ya wagonjwa
wa nje, hivyo tunahitaji eneo kubwa zaidi ili tuweke majengo mengi kwa lengo la
kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi,” ameongeza.
Akizungumza katika hatua nyingine mara baada
ya kuzindua majengo ya Shule ya Msingi Kigamboni katika Halmashauri ya Wilaya
ya Tabora, Mhe. Kikwete amesema Sera ya Elimu ni kuhakikisha vijana wanapata
elimu jirani badala ya kutembea umbali mrefu.
Amesema lengo la Serikali ni kupunguza adha
ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu na ndio maana inajenga shule
jirani ili wapate muda mrefu wa kusoma badala ya kutumia muda huo kutembea.
Aidha, ameongeza kuwa wingi wa majengo
unasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi kurundikana kwenye darasa moja na
kuwarahisishia Walimu kufundisha na wanafunzi kupata uelewa.
“Zamani wakati sisi tunasoma, darasa moja
lilikuwa na wanafunzi wengi kwasababu madarasa yalikuwa machache, lakini sasa
hivi madarasa mengi hivyo wanafunzi katika darasa moja hawazidi 45, aidha
Walimu wanapata muda wa kuwa na wanafunzi karibu wanaoweza kuwamudu, wanafunzi
sasa hivi mtake wenyewe kufeli,” ameongeza.
Amesema akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana wa
masuala ya Utumishi, atahakikisha anasimamia zoezi la kupatikana kwa Walimu wa
kutosha ili wanafunzi wapate elimu bora.
“Majengo yamejengwa, ni mazuri, hata sehemu
nyingine mjini hakuna majengo kama haya, hivyo wanafunzi muhakikishe mnafanya
vizuri katika masomo yenu, tutaleta Walimu ili watoto wapate elimu bora huku
akisisitiza utunzaji wa majengo hayo ili yadumu muda mrefu.
Suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo
amelisisitiza tena wakati akikagua na kuzindua kituo cha afya cha Maili Tano
katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
“Hongereni kwa kazi nzuri, kikubwa
niwasisitize usimamizi katika miradi hii kama nilivyosema hapo awali, ili
thamani ya fedha ionekane,” ameongeza.
Mhe. Ridhiwani amehitimisha ziara yake kwa
siku ya leo kwa kuzungumza na Wananchi Manispaa ya Tabora ambapo alipata fursa
pia ya kusikiliza changamoto zao kwa
lengo la kuzifanyia kazi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge baada ya kuweka jiwe la msingi
katika kituo cha afya cha Igigwe wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika
kituo cha afya cha Igigwe wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadili jambo na Watendaji wa Mkoa wa Tabora baada
ya kukagua na
kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Mwonekano wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) lililopo katika kituo
cha afya cha Maili Tano, katika Halmashauri
ya Manispaa ya Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akielekea kukagua jengo la Kitengo cha Tiba na Mionzi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi, Watendaji, Madaktari na Wananchi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akishauri jambo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Tabora, Bi. Asha Churu wakati Waziri huyo ali[powasili katika Halmashauri ya Wilaya Tabora kukagua na kuzindua majengo ya Shule ya Msingi Kigamboni wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kuhusu
maabara ya kituo cha afya cha Igigwa wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Sehemu
ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigamboni wakimsikilza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akipiga makofi mara baada ya kuzindua kituo cha
afya cha Maili Tano kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa mkoa huo.
Mwonekano wa jengo la Kitengo cha Tiba na Mionzi lililopo katika kituo cha afya cha Maili Tano, katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Mwonekano wa jengo la kituo cha afya cha Igigwa kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Mwonekano wa jengo la Shule ya Msingi Kigamboni lililopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Tabora
MHE. KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA AFYA NA DARAJA IGUNGA ASISITIZA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA
Na. Veronica Mwafisi-Igunga
Tarehe 08 Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila na daraja la Nyandekwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora huku akisisitiza kuilinda amani
ya nchi kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti leo tarehe 08
Julai, 2026 katika maeneo hayo, Mhe.
Kikwete amesema maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na ujenzi wa
daraja hilo yasingekuwepo kama kungekuwa hakuna amani.
“Tuendelee kufanya kazi kwa bidii, tuitunze
amani ya nchi yetu, tumekusanyika hapa kwasababu tuna amani hivyo tusikubali
kurubuniwa kuivuruga amani ya nchi yetu.” Amesisitiza.
Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya
Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuweka kipaumbele katika
maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, miundombinu, maji lengo ni
kutaka wananchi wafurahie matunda ya nchi yao.
“Kituo hiki cha afya cha KiningÃnila ni
mwanzo tu, kwani mpango wa Serikali ni kujenga majengo mengi zaidi ili mpate
huduma mbalimbali ikiwemo ya afya ya mama na mtoto, huduma ya meno na nyingine
nyingi,” amesisitiza
Aidha, amesema katika Mkoa wa Tabora, Serikali
imeajiri watumishi 2200 ikiwemo watumishi wa afya ili wananchi waweze kupata
huduma za kitabibu kama ilivyo katika maeneo mengine.
Kuhusu ujenzi wa daraja la Nyandekwa, Mhe.
Kikwete amesema daraja hilo litaenda kuondoa adha ya muda mrefu ya kivuko iliyokuwa
ikikwamisha shughuli za maendeleo ya wakazi wa Kijiji cha Manonga na maeneo
jirani.
Amesema Mhe. Rais alitoa fedha zaidi ya
milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ili kutatua changamoto ya
kivuko.
Mhe. Kikwete ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Tabora inayolenga kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakati wa
ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mara baada ya kuweka jiwe la
Msingi katika daraja la Nyandekwa mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitoka kukagua daraja la
Nyandekwa wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri
hiyo.
Wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
alipokuwa akizungumza nao mara baada ya
kuweka jiwe la Msingi katika daraja la Nyandekwa mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la
msingi daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Dkt. Lucia Kafumo alipokuwa akimueleza jambo
baada ya Waziri huyo kukagua Mradi wa ujenzi wa
kituo cha afya cha Kining’inila katika Halmashauri
ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora
wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akikagua Daraja daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na
kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi
na Wananchi wa Halmashauri hiyo.
Mwonekano wa daraja la Nyandekwa lililopo katika kata ya Nyandekwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani
Tabora.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika Daraja daraja la Nyandekwa katika Halmashauri
ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora
wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwonekano wa Nyuma Mradi
wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila
kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Igunga mkoani Tabora.
MHE. KIKWETE AWASILI MKOANI TABORA KWENYE ZIARA YAKE YA KIKAZI
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora tayari kuanza ziara
yake ya kikazi iliyolenga kukagua,
kuzindua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
kusikiliza changamoto za wananchi katika Mkoa huo.
Tuesday, July 7, 2026
MHE. RIDHIWANI AZINDUA NYUMBA ZA WATUMISHI NZEGA ASISITIZA UTENDAJI KAZI
Na. Veronica Mwafisi-Nzega
Tarehe 08 Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua nyumba mbili
za Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Mji Nzega na kuwasisitiza kufanya kazi
kwa bidii na weledi katika kuwatumikia wananchi.
Mhe. Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 08
Julai, 2026 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Nzega
baada ya kuzindua ujenzi wa nyumba hizo zilizojengwa jirani na ofisi za
Halmashauri hiyo.
“Tunayoyaona hapa ni ushuhuda tosha kwamba
Serikali imekuwa ikiwajali watumishi wake, nyumba hizi zimejengwa kwa ustadi wa
hali ya juu, ni nzuri sana, ziko kwenye mazingira mazuri, haya yanatekelezwa
ili mfanye kazi kwa bidii,” amesisitiza.
Amesema amekuwa akipata barua za mara kwa
mara za watumishi wanaoomba uhamisho, “hali hii hainifurahishi hata kidogo na
ndio maana Serikali imekuwa ikijitahidi kuweka mazingira mazuri ili mtulie
kwenye vituo vyenu vya kazi, ukikaa kwenye nyumba kama hii huwezi kufikiria
kuhama,” amesema.
Amesema Serikali imekuwa ikishughulikia
changamoto mbalimbali za watumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa umma,
akitolea mfano upandishwaji wa madaraja na malipo ya stahiki mbalimbali, huku
akiwasisitiza waajiri kulipa madai ya watumishi na kuongeza kuwa Serikali
itaendelea kuwajali Watumishi wa Umma wakati wote.
Ameongeza kuwa, maelekezo ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watumishi wanatatuliwa changamoto
zinazowakabili ili waweze kuwatumikia wananchi kwa ufasaha, hivyo hakuna sababu
ya Waajiri kutoshughulikia changamoto za watumishi.
Mhe. Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya
siku tatu aliyoianza leo mkoani Tabora ambapo ametembelea katika Halmashauri ya
Wilaya ya Igunga na Halmashauri ya Mji Nzega kwa lengo la kukagua shughuli za
maendeleo katika halmashauri hizo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa
Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (aliyevaa shati jeupe) akipiga makofi mara baada ya kuzindua nyumba mbili za Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Mji
Nzega wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa mkoa huo.
Mwonekano wa nyumba mojawapo ya Wakuu wa Idara iliyojengwa katika Halmashauri
ya Mji Nzega mkoani Tabora.
Viongozi,
Watendaji na Wananchi wa Halmashauri ya Mji
Nzega wakishuhudia uzinduzi wa nyumba mbili (hazipo pichani) za Wakuu wa Idara
katika Halmashauri hiyo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipozizindua baada ya
kuzikagua wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tabora.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (wapili kutoka kushoto) akifurahia jambo wakati akikagua
nyumba za Wakuu wa Idara katika Halmashauri
ya Nzega wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Halmashauri hiyo mkoani Tabora. Wa
kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (aliyevaa shati jeupe meza kuu) akipokea taarifa kuhusu
utekelezaji wa ujenzi wa nyumba mbili za Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Nzega wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Halmashauri hiyo mkoani Tabora.

























