Na. Antonia Mbwambo–Kigoma
Tarehe 2 Julai, 2026
Serikali
imeeleza kuridhishwa na Maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Nyumba
za Watumishi wa Umma Awamu ya Pili katika Mkoa wa Kigoma kufuatia ukaguzi
uliofanywa na timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investimentsl.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Bw. Patrick
Allute, wakati wakihitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya makazi ya Watumishi
wa Umma Mkoani Kigoma ambapo timu ilikagua mradi ya nyumba za Watumishi katika
Shule ya Sekondari Muhunga, Wilaya ya Kasulu, na Kituo cha Afya Muyama, Wilaya
ya Buhigwe,Mkoa wa Kigoma
Akizungumza
baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Bw. Allute amepongeza wasimamizi wa mradi,
Watumishi Housing na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa usimamizi unaowezesha
miradi hiyo kutekelezwa kwa ufanisi. Amesema hatua iliyofikiwa inaakisi dhamira
ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuboresha mazingira ya kazi na
ustawi wa Watumishi wa Umma.
Aidha,
ameutaja mradi wa nyumba za Watumishi katika Kituo cha Afya Muyama kuwa
miongoni mwa miradi iliyofanya vizuri zaidi kati ya miradi 15 iliyokaguliwa
katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania kutokana na kasi ya utekelezaji na ubora wa
kazi inayoendelea kuonekana.
"Mradi
wa nyumba za Watumishi katika Kituo cha Afya Muyama umeonesha kiwango cha juu
cha utekelezaji. Kazi nyingi muhimu, ikiwemo mfumo wa umeme, zimekamilika na
mradi umebakiza hatua chache kabla ya kukamilika na kuanza kutumika," amesema Bw. Allute.
Kwa
upande wake, Msimamizi wa Mradi wa Kituo cha Afya Muyama ameishukuru timu ya
ukaguzi kwa ushauri na maelekezo yaliyotolewa, akisema yataendelea kufanyiwa
kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa Watumishi
wa Umma waliokusudiwa kunufaika nao.
Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais–UTUMISHI na
Watumishi Housing
Investment (WHI) wakijadili jambo mara baada ya kufanya
ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
Timu
ya wataalamu kutoka Ofisi
ya Rais–UTUMISHI na Watumishi
Housing Investment (WHI) wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu
Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Muyama Bw. Kwima Juma Buanza (wa tatu kutoka
kushoto), mara baada ya timu hiyo kukamilisha ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa
nyumba za watumishi wa kituo hicho kiiilichopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa
Kigoma.
Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji kutoka Watumishi
Housing Investiment (WHI) Bw. Paskali Massawe (aliyenyoosha mkono)
akielezea jambo kwa Wataalamu alioambatana nao katika ukaguzi wa mradi wa
ujenzi wa Kituo
cha Afya Muyama, Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, mara baada ya kufika kwenye
eneo hilo Julai 2, 2026
Wataalamu
kutoka Ofisi ya
Rais–UTUMISHI na Watumishi
Housing Investment (WHI) wakijadili jambo mara baada ya
kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya
Watumishi wa Shule ya Sekondari Muhunga iliyopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa
Kigoma.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Patrick Allute (wa
tano kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti,
wa Ofisi hiyo, Bi. Julieth Magambo
wakati
wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya watumishi wa Shule ya
Sekondari Muhunga iliyopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Wataalamu
kutoka Ofisi ya
Rais–UTUMISHI na Watumishi
Housing Investment (WHI) wakijadili jambo mara baada ya
kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya
Watumishi wa Shule ya Sekondari Muhunga iliyopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa
Kigoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na
Tathmini, Bw. Patrick
Allute, (aliyenyoosha mikono), akitoa maelekezo kwa Makamu Mkuu
wa Shule ya Sekondari Muhunga Mwl. Beatus Damiani,(wa pili kutoka kushoto) wakati
wa ukaguzi wa SHule hiyo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoa wa
Kigoma, leo tarehe 2 Julai, 2026.
Muonekano wa
mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma Shule ya Sekondari
Muhunga iliyopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Patrick Allute (wanne kutoka kushoto) akiagana na Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwl. Jeremiah Ntiboneka mara baada ya Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais–UTUMISHI na Watumishi Housing Investment (WHI) kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Muhunga iliyopo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

No comments:
Post a Comment