Na. Veronica Mwafisi-Uyui
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan anatambua changamoto ya ajira katika sekta mbalimbali
ikiwemo elimu na ndio maana kati ya vipaumbele vya Serikali vilivyopo, ajira ni
mojawapo.
Mhe. Kikwete amesema hayo leo tarehe 10
Julai, 2026 wakati akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi
katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora kabla ya kukagua na kuzindua
Shule ya Msingi Ilolangula Mlimani katika Wilaya hiyo.
“Serikali inafahamu changamoto ya ajira hususan
katika sekta ya Elimu na Afya na ndio maana Rais wetu mpendwa amekuwa akitoa
vibali vya ajira, huku akifafanua kuwa mwaka huu wa fedha 2026/27 kibali cha
ajira kwa watumishi 45,000 kimetolewa ambapo Sekta ya Elimu itafaidika pia,”
amesisitiza Mhe. Kikwete.
Ameongeza kuwa haya yote yanafanyika
kwasababu Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa
akiwajali wananchi wake hasa katika kupata huduma bora huku akiwasisitiza
wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwani elimu ni muhimu kwa maendeleo ya
mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
“Suala la elimu linasisitizwa sana hata
katika vitabu vyote vitakatifu vya dini, hivyo wanafunzi hamna budi kusoma kwa
bidii ili kuwa na ufahamu wa mambo mengi kwa maendeleo ya taifa letu,”
ameongeza.
Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amuelekeza
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutenga
bajeti kwa ajili ya kujenga Ofisi ya TAKUKURU wilayani Uyui.
Amesema Ofisi ya TAKUKURU ina umuhimu wake
katika kuzuia na kupambana na rushwa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa
katika Wilaya hiyo.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mhe. Mohamed
Mtulyakwaku aliwasilisha changamoto kwa Mhe. Waziri Kikwete kuwa Wilaya yake
inakabiliwa na uhaba wa Watumishi hasa katika Sekta ya Elimu na Afya, hivyo
aliiomba Serikali kuwapatia watumishi hao ili waweze kuwadumia wananchi
kikamilifu.
“Tunatambua kuwa Serikali imekuwa ikituletea
watumishi wapya lakini bado tuna uhitaji, hivyo tunaomba mtufikirie katika
hili,” aliongeza Mkuu wa Wilaya huyo.
Aidha, alizungumzia suala la kutokuwepo kwa
Ofisi ya TAKUKURU katika Wilaya hiyo kwani wamekuwa wakisafiri mpaka Tabora
mjini kufuata huduma hiyo pale wanapoihitaji.
Waziri Ridhiwani Kikwete anahitimisha leo ziara
yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza
na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi
katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kabla ya kukagua
na kuzindua Shule ya Msingi lolangulu Mlimani katika Wilaya hiyo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia)
akiteta jambo na Mwakilishi wa
Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhe. Upendo Wella wakati wa ziara ya
kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na
kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora
Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua na kuzindua Shule ya Msingi lolangula Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyevaa
miwani) akielekea kukagua na kuzindua Shule ya
Msingi lolangulu Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wapili
kutoka kushoto) akiweka jiwe la msingi mara baada ya kukagua na kuzindua Shule ya Msingi lolangula Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Tabora
Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani)
alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua na
kuzindua Shule ya Msingi lolangulu Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na
kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Tabora.
Sehemu ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi lolangula Mlimani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa
akizungumza baada ya kukagua na
kuzindua Shule ya Msingi lolangulu Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Tabora.
Watumishi wa Umma na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua na kuzindua Shule ya Msingi lolangulu Mlimani wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta
jambo na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mhe. Shabani Katalambula wakati wa ziara ya kikazi ya
Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.



No comments:
Post a Comment