Na. Veronica Mwafisi-Tabora
Tarehe 11
Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaelekeza Waajiri katika Sekta ya Umma
mkoani Tabora kufanyia kazi madai ya watumishi ili waweze kutekeleza majukumu
yao kwa ufasaha.
Akifanya kikao cha majumuisho na Viongozi na Watumishi wa Umma wa
Mkoa wa Tabora leo tarehe 11 Julai, 2026 baada ya kuhitimisha ziara yake ya
kikazi ya siku tatu katika mkoa huo, Mhe. Kikwete amesema katika mwaka huu wa
fedha Waajiri washughulikie masuala yote ya kiutumishi ikiwemo kupanda
madaraja, kulipa malimbikizo, kuwabadilisha kada wanaostahili pamoja na madai
mengine.
Amesema Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali ya
watumishi kuhusiana na kutoshughulikiwa stahiki zao jambo ambalo limekuwa
likishusha ari ya utendaji kazi na kushindwa kuwahudumia wananchi kikamilifu.
“Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi
wake wapate huduma bora, mwaka huu wa fedha tushughulikie changamoto zote za
watumishi ili watoe huduma kwa furaha,” amesisiza.
Kuna watumishi wana sifa ya kupandishwa madaraja, wengine
kubadilishiwa kada na wengine wana madai yao mbalimbali. “Ninaelekeza wote
wanaostahili watekelezewe na kama kuna changamoto yoyote mnayokutana nayo
katika utekelezaji wa hili mtuletee Ofisini tuone namna ya kulitatua,”
ameongeza
Aidha, amewataka Maafisa Rasilimaliwatu kutoa ushauri kwa Waajiri
utakaosaidia kutatua changamoto za kiutumishi.
Amesema changamoto za kiutumishi zikishindwa kutatuliwa basi wa
kulaumiwa si mwingine bali ni Maafisa Rasilimaliwatu kwani wanayo nafasi kubwa
ya kutoa ushauri mzuri kulingana na taaluma zao.
Mhe. Kikwete amewapongeza Viongozi na Watumishi wa Mkoa huo kwa
ushirikiano mzuri baina ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi uliochangia
utekelezaji mzuri wa majukumu ya miradi ya maendeleo.
“Tunatekeleza Ilani ya
Chama kilichoko madarakani, niwapongeze kwa ushirikiano baina yenu, endeleeni
kufanya kazi kwa pamoja kwani ndio msingi wa maendeleo ya taifa letu,”
ameongeza
Vile vile Waziri Kikwete ametoa wito kwa Viongozi na Watumishi wa
Mkoa huo kuzungumza na wananchi ikiwemo vijana na kusikiliza changamoto zao
badala ya kusubiria viongozi wengine kutoka maeneo ya mbali kuzungumza.
Amesema kujua changamoto za vijana hao kunasaidia kwani wengine
unakuta wanahitaji kitu kidogo cha kujiendeleza kiuchumi na kumuepusha kuingia
katika masuala yasiyo na maadili.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Tabora, Bi. Upendo Wella amemshukuru Mhe. Kikwete kwa ziara
aliyoifanya katika mkoa huo ambayo itaenda kuboresha utendaji wa Watumishi kwa
maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Tabora baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu ya Viongozi,
Watumishi wa Umma na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa
huo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu ya Viongozi na Watumishi wa Umma wa Mkoa
wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara
yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waheshimiwa
Wabunge wa Mkoa wa Tabora, Viongozi na Watumishi
wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara
yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa
huo iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao baada ya kuhitimisha ziara
yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo iliyolenga kukagua na kuzindua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.






No comments:
Post a Comment