Na.
Veronica Mwafisi-Urambo
Tarehe 10
Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewakumbusha Waajiri katika Taasisi za
Umma kutilia mkazo suala la msawazo kwa Watumishi ili kupunguza changamoto ya
uhaba wa watumishi katika maeneo mbalimbali kwenye sekta hiyo ya umma kwa lengo
la kuwatumikia wananchi kwa ufasaha.
Mhe. Kikwete amesema hayo leo tarehe 10 Julai, 2026 wakati
akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi katika Halmashauri ya
Wilaya ya Urambo mkoani Tabora baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke.
Amesema kabla ya Waajiri kulalamika changamoto ya uhaba wa
watumishi, ni vema wakakaa na kufanya msawazo ili kujiridhisha kama kweli wana
changamoto hiyo katika maeneo yao kabla ya kuomba kupatiwa watumishi wapya.
“Utakuta kuna taasisi watumishi wa kada fulani wamerundikana
katika kituo kimoja cha kazi huku kituo cha kazi cha jirani kina uhaba wa
watumishi wa kada hiyo, au Waajiri kaeni, fanyeni msawazo, kabla ya kulalamikia
changamoto hiyo ya uhaba wa watumishi,” ameongeza Mhe. Kikwete.
Ameongeza kuwa kuna taasisi unakuta kuna watumishi wa kada fulani
ambao sio hawahitajiki sana katika taasisi fulani kutokana na majukumu yake
lakini wapo huku taasisi yenye uhitaji wa watumishi wa kada hiyo hakuna.
Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amewataka wananchi wa Kata ya Usoke kukitunza kituo cha Polisi kinachojengwa katika kata hiyo ili kiwasaidie katika kupambana na uhalifu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha Polisi Usoke wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza
kulia) akiwa katika mkutano mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akikata
utepe kuzindua ujenzi wa kituo cha Polisi
Usoke katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo baada ya kukagua na kuweka jiwe la
msingi wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyevaa
miwani) akipiga makofi mara baada ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke,
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisikiliza
taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo
cha Polisi Usoke katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kabla ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.
Viongozi, Watumishi wa Umma na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi Usoke, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Tabora.





No comments:
Post a Comment