Na. Veronica Mwafisi-Igunga
Tarehe 08 Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila na daraja la Nyandekwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora huku akisisitiza kuilinda amani
ya nchi kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti leo tarehe 08
Julai, 2026 katika maeneo hayo, Mhe.
Kikwete amesema maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na ujenzi wa
daraja hilo yasingekuwepo kama kungekuwa hakuna amani.
“Tuendelee kufanya kazi kwa bidii, tuitunze
amani ya nchi yetu, tumekusanyika hapa kwasababu tuna amani hivyo tusikubali
kurubuniwa kuivuruga amani ya nchi yetu.” Amesisitiza.
Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya
Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuweka kipaumbele katika
maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, miundombinu, maji lengo ni
kutaka wananchi wafurahie matunda ya nchi yao.
“Kituo hiki cha afya cha Kiningínila ni
mwanzo tu, kwani mpango wa Serikali ni kujenga majengo mengi zaidi ili mpate
huduma mbalimbali ikiwemo ya afya ya mama na mtoto, huduma ya meno na nyingine
nyingi,” amesisitiza
Aidha, amesema katika Mkoa wa Tabora, Serikali
imeajiri watumishi 2200 ikiwemo watumishi wa afya ili wananchi waweze kupata
huduma za kitabibu kama ilivyo katika maeneo mengine.
Kuhusu ujenzi wa daraja la Nyandekwa, Mhe.
Kikwete amesema daraja hilo litaenda kuondoa adha ya muda mrefu ya kivuko iliyokuwa
ikikwamisha shughuli za maendeleo ya wakazi wa Kijiji cha Manonga na maeneo
jirani.
Amesema Mhe. Rais alitoa fedha zaidi ya
milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ili kutatua changamoto ya
kivuko.
Mhe. Kikwete ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Tabora inayolenga kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakati wa
ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mara baada ya kuweka jiwe la
Msingi katika daraja la Nyandekwa mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akitoka kukagua daraja la
Nyandekwa wakati
wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri
hiyo.
Wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
alipokuwa akizungumza nao mara baada ya
kuweka jiwe la Msingi katika daraja la Nyandekwa mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la
msingi daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi na Wananchi wa Halmashauri hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Dkt. Lucia Kafumo alipokuwa akimueleza jambo
baada ya Waziri huyo kukagua Mradi wa ujenzi wa
kituo cha afya cha Kining’inila katika Halmashauri
ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora
wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akikagua Daraja daraja la Nyandekwa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na
kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Wengine ni Viongozi
na Wananchi wa Halmashauri hiyo.
Mwonekano wa daraja la Nyandekwa lililopo katika kata ya Nyandekwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani
Tabora.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika Daraja daraja la Nyandekwa katika Halmashauri
ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora
wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwonekano wa Nyuma Mradi
wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kining’inila
kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Igunga mkoani Tabora.







No comments:
Post a Comment