Na. Veronica Mwafisi-Tabora
Tarehe 11
Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaambia wanafunzi wa Shule ya Sekondari
ya Wavulana Tabora kuishi katika maadili wawapo shuleni na hata baada ya
kumaliza shule ili wajiepusha na tabia ambazo zitawafanya wajiingize katika
makundi yasiyofaa ya uvunjivu wa amani.
Mhe. Ridhiwani amesema hayo leo tarehe 11 Julai, 2026
alipotembelea shule hiyo kabla ya kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi
ya siku tatu mkoani Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu
mkoani humo.
Amesema kuna maisha baada ya kumaliza shule, hivyo wanafunzi hao
wanatakiwa wakawe mfano mzuri katika maadili na uzalendo kwa wengine huko
wanakoenda kutokana na sifa za shule hiyo.
“Shule hii imetoa viongozi wengi sana, waadilifu na wazalendo,
hivyo mtunze heshima yake, mkajitofautishe na wengine, msiige tabia ambazo sio
nzuri,” amesisitiza.
Amepongeza uongozi wa shule hiyo kwa matokeo mazuri ya kidato cha
sita mwaka huu na miaka iliyopita na ufaulu mzuri pia hata kwa kidado cha nne
na kuwasihi kuendelea kufanya vizuri zaidi ili elimu hiyo iwakomboe wao binafsi
na taifa kwa ujumla.
Aidha, ametoa wito kwa Viongozi wa Mkoa wa Tabora kuwa karibu na
wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine zote ili wawasaidie kukua kimaadili.
“Watoto hawa ni wadogo, tuwasaidie hata watakapotoka hapa waendelee kuwa na sifa nzuri huko watakakokwenda.






No comments:
Post a Comment