Na. Veronica Mwafisi-Kaliua
Tarehe 10 Julai, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa mradi wa maji unaosuasua katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaliua katika mkutano wa
hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za maendeleo mkoani Tabora, Waziri Kikwete amesema Wilaya hiyo ina
changamoto kubwa ya maji na Mkandarasi amechukua muda mrefu kukamilisha mradi
huo.
“Najua kuwa changamoto kubwa katika eneo hili ni pamoja na maji,
Mhe. Mbunge umeeleza vizuri juu ya mradi wa maji wa Ichemba ambao ulitegemewa
kutatua changamoto ya maji, maagizo yangu, hatuwezi kuwa na mradi wa miaka 15,
wananchi hawa wavuja jasho wanaumia kwa kusosa maji, sisi viongozi na
wasimamizi hatuwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote kwa kuona ni kawaida
tu, Kamanda wa TAKUKURU ninakuelekeza uchunguzi wa kina ufanyike kubaini tatizo
liko wapi na likishabainika hatua za kisheria zifuate mkondo wake,”
amesisitiza.
Amesema Serikali itatafuta mtu mwingine wa kumalizia mradi huo ili
ukamilike na wananchi waweze kunufaika na kuongeza kuwa, ni jukumu lake na
viongozi wengine wanaosimamia maeneo ya utawala kuhakikisha fedha za wananchi
zinatumika vizuri na thamani yake inaonekana.
Waziri Kikwete amehitimisha ziara yake leo kwa kukagua, kuzindua
na kuweka jiwe la msingi miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Uyui,
Urambo na Kaliua mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi Wilaya ya Kaliua katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku
tatu ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo mkoani Tabora.
Sehemu ya Wananchi katika Wilaya ya Kaliua wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa
hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiandika jambo wakati alipokuwa kwenye akihitimisha mkutano wa
hadhara kwenye ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa shughuli za
maendeleo mkoani Tabora.
Sehemu ya Wananchi katika Wilaya ya Kaliua wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa
hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za maendeleo mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mhe. Dk. Rashid Chuachua (kulia) kwenye mkutano wa hadhara wakati Waziri huyo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo mkoani Tabora.
Sehemu ya Wananchi katika Wilaya ya Kaliua wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa
hadhara wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa
shughuli za maendeleo mkoani Tabora.

No comments:
Post a Comment