Wednesday, July 22, 2026

WARATIBU WA KUDHIBITI VVU, UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA WATAKIWA KUTOA ELIMU JUU YA UDHIBITI MAGONJWA MAHALI PA KAZI ILI KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

 Veronica Mwafisi -Dodoma

Tarehe 22 Julai, 2026

Waratibu wa ngazi ya Mikoa Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma wametakiwa Kutoa elimu kwa watumishi wa umma juu ya udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga taifa lenye watu wenye afya, tija, ustawi na ufanisi ambao watatoa huduma bora kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato wakati akifungua semina elekezi kwa Waratibu wa ngazi ya Mikoa kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Kato amesema katika kutekeleza afua za kuimarisha afya kwa watumishi ni vema kuwa na program za upimaji wa afya pamoja na mazoezi ya viungo kwa watumishi katika maeneo yao ya kazi ili kufikia utekelezaji huo wa Dira 2050.

Ameongeza kuwa, itakuwa vema kuandaa mafunzo pia kwa watumishi pamoja na msaada wa kisaikolojia ili kuwasaidia zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao.   

Aidha, Dkt. Kato amewataka waratibu hao kuandaa taarifa za utekelezaji wa Mwongozo na Waraka Na. 2 wa mwaka 2014 kuhusu kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu, Bi. Herieth Mpili akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kukuza uelewa na ufahamu juu ya majukumu ya Waratibu hao na kuwawezesha kuandaa mipango ya muda mrefu na mfupi wa utekelezaji wa afua za kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa yote nchini kwa lengo la kusimamia masuala ya Anuai za Jamii na kutoa mafunzo kwa maafisa au waratibu watakaoteuliwa kuratibu afua hizo katika mikoa yao ili kuhakikisha kunakuwa na afya imara na ustawi wa watumishi wote nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato akizungumza na Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakati wa semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakimsikiliza, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato wakati akifungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakimsikiliza, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato wakati akifungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu, Bi. Herieth Mpili akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Charles Kato kuzungumza na Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakati wa semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Afisa Maendeleo ya Jamii, Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Neema Range akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Anuai za Jamii na Ujumuishwaji wa Mwongozo Wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na MSY na Waraka (2014) kwa Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakati wa semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Bingwa wa Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Garvin Kweka akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Afya ya Akili kwa Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma. 


Mratibu wa ngazi ya Mkoa kutoka Kagera ambaye ni Afisa Rasilimaliwatu Mkuu, Bw. Emily Ishegoma akiwasilisha maoni yake wakati wa majadiliano kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Mwakilishi kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Theresiaglory Tety akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Hali Halisi kuhusu VVU na UKIMWI wakati wa semina elekezi kwa Waratibu wa ngazi ya Mikoa iliyoandaliwa na Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa ngazi ya Mikoa mara baada ya kufungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa ngazi ya Mikoa mara baada ya kufungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Maafisa kutoka Idara ya Uendelezaji Sera, Sehemu ya Menejimenti Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia jambo wakati wa semina elekezi kwa Waratibu wa ngazi ya Mikoa kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI mara baada ya kufungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Waratibu wa ngazi ya Mikoa wakimsikiliza, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera wa ofisi hiyo, Dkt. Charles Kato wakati akifungua semina elekezi kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.





 

No comments:

Post a Comment