Friday, May 30, 2014

Utumishi yawapongeza wafanyakazi bora wa mwaka 2014

Katibu Mkuu-Utumishi Bw.George D. Yambesi akitoa pongezi kwa watumishi bora wa ofisi yake.Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu - Utumishi Bw. HAB Mkwizu na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi Bw. Abdulrahman Msabila.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na RasilimaliwatuUtumishi Bw. Aloyce Msigwa akiongea katika hafla fupi ya kutoa zawadi kwa Watumishi bora wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu-Utumishi Bw.George D. Yambesi  (hayupo pichani) wakati akiitoa pongezi kwa watumishi hao. 

Dkt.Fidelis Owenya kutoka GIZ akitoa mada kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi .

Katibu Mkuu - Utumishi Bw.George D. Yambesi akimkabidhi zawadi Mfanyakazi Bora wa Kitengo Ukaguzi wa Ndani Bw. George Manyai katika hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora.

Katibu Mkuu - Utumishi Bw.George D. Yambesi akimkabidhi zawadi Mfanyakazi Bora wa Kitengo Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ndani Bi. Judith Ntiyangiri katika hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora.

Katibu Mkuu-Utumishi Bw.George D. Yambesi (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2014 baada ya hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika ofisini hapo .

Thursday, May 29, 2014

FURSA YA UFADHILI WA MASOMO NCHINI JAPANI 2015

Ungependa kusoma nchini Japani?

Maombi yako yanatakiwa kutumwa kabla ya tarehe 16 Juni, 2014

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ifuatayo; www.utumishi.go.tz