Thursday, April 18, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2019

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi yake wakati wa kikao cha uchaguzi wa mfanyakazi bora kilichofanyika jijini Dodoma.  Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsilikiza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) alipokuwa akitangaza mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Utumishi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimpa mkono wa pongezi mfanyakazi bora wa mwaka 2019 wa ofisi yake Bw. Jafari Kalaghe, Afisa Tawala baada ya uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa tayari kuwasilisha kura yake baada ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni  Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw Ayoub Banzi na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Mary Mwakapenda.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akisimamia zoezi la kuhesabu kura kwa ajili ya kumchagua wa mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni wawakilishi wa wafanyakazi bora walioingia kwenye ushindani.


Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akifafanua jambo kwa watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge.
Baadhi ya wafanyakazi bora wa Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akitoa ufafanuzi wa kanuni za kumchagua mfanyakazi bora kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni  Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Musa Joseph.
Monday, April 15, 2019

UJUMBE KUTOKA KWA DKT. LAUREAN NDUMBARO KWA WANANCHI NA WADAU WOTE WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA


UTUMISHI YAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, akifurahia jambo na wasaidizi wake baada ya ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.Thursday, April 11, 2019

MHE. MKUCHIKA AWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Taasisi zilizo chini yake.
 


UJUMBE WA MHE. MKUCHIKA KWA WAAAJIRI WA TAASISI ZA UMMA NCHINI


WAHITIMU WA MAFUNZO YA UONGOZI WATAKIWA KUTUMIA VIZURI UJUZI WALIOUPATA ILI KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi inayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha AALTO cha nchini Finland, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimpongeza mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Leonce Temba baada ya kuhitimu mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi inayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha AALTO cha nchini Finland, baada ya hafla ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.