Thursday, April 18, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2019

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi yake wakati wa kikao cha uchaguzi wa mfanyakazi bora kilichofanyika jijini Dodoma.  Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsilikiza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) alipokuwa akitangaza mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Utumishi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimpa mkono wa pongezi mfanyakazi bora wa mwaka 2019 wa ofisi yake Bw. Jafari Kalaghe, Afisa Tawala baada ya uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa tayari kuwasilisha kura yake baada ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni  Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw Ayoub Banzi na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Mary Mwakapenda.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akisimamia zoezi la kuhesabu kura kwa ajili ya kumchagua wa mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni wawakilishi wa wafanyakazi bora walioingia kwenye ushindani.


Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akifafanua jambo kwa watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge.
Baadhi ya wafanyakazi bora wa Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akitoa ufafanuzi wa kanuni za kumchagua mfanyakazi bora kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni  Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Musa Joseph.




No comments:

Post a Comment