Monday, June 30, 2014

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atembelea Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu (NRC) Dodoma

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Kituo cha Taifa cha Utunzaji  Kumbukumbu (NRC) Dodoma leo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (kushoto), pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi wakipitia moja ya jalada lililofunguliwa mwanzoni mwa miaka ya 60.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (wa kwanza kulia) katika moja ya sehemu za kuhifadhi kumbukumbu katika Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu, kushoto kabisa anayetoa maelezo  ni Mkurugenzi Msaidizi Utumishi Bw. Joseph Ndauka.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi akitoa maelezo mafupi kuhusu Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu (NRC) Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue  (hayupo pichani) katika Kituo cha Taifa cha Utunzaji Kumbukumbu (NRC) Dodoma.

Saturday, June 28, 2014

AAPAM TANZANIA CHAPTER YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA

Mlezi wa AAPAM Tanzania Chapter Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi akifungua mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter katika ukumbi wa mikutano wa  St.Gaspar mjini Dodoma leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (hayupo pichani) akifungua mkutano huo.

Katibu wa AAPAM Tanzania Chapter Bi.Roxana Kijazi (katikati) akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter katika ukumbi wa mikutano wa St.Gaspar mjini Dodoma leo. Wengine ni mjumbe wa kamati ya utendaji AAPAM Tanzania Chapter Amos Nnko (kulia), Makamu Mwenyekiti wa AAPAM Tanzania Chapter Bi. Ellyn Mcha (wa tatu kutoka kulia)  na Mlezi wa AAPAM Tanzania Chapter Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto).

Mmoja wa wajumbe wa AAPAM Tanzania Chapter Bi. Victoria Fovo akichangia mada wakati wa mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter katika ukumbi wa mikutano wa St.Gaspar mjini Dodoma leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (hayupo pichani) akifungua mkutano huo.

Mweka Hazina wa AAPAM Tanzania Chapter Bi. Emma Lyimo akisoma taarifa ya mapato na matumizi kwenye mkutano wa mwaka wa AAPAM Tanzania Chapter katika ukumbi wa mikutano wa St.Gaspar mjini Dodoma leo.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA UTAWALA NA RASILIMALIWATU SERIKALINI WAFUNGWA RASMI

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gaspar mjini Dodoma .

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (hayupo pichani) kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gaspar mjini Dodoma .

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala (kulia) akiongea kabla ya kufungwa kwa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gaspar mjini Dodoma.Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu, Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi na Mkurugenzi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw.Nyakimura Muhoji.

Friday, June 27, 2014

WAAJIRI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifuatilia mada mjini Dodoma leo.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga  kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa  za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.

“Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao  wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw.Robert.

Alisema, mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Aidha,Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Bw.Robert alifafanua kuwa ili kufanikisha zoezi la urejeshaji  mikopo kutoka kwa wadaiwa,  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatunga sheria na mifumo  mbalimbali ya kuwadhibiti wadaiwa hao.

“Tunatengeneza sheria ambazo zitawazuia wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kupata hati ya kusafiria nje ya nchi au kibali cha kusafiri hadi atakapowasiliana na Bodi.”
Pia,alisema mhitimu atakayeshindwa kulipa mkopo taarifa zake zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye taasisi za mikopo ili asipate huduma yoyote ya kifedha.
Naye, Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Dk. Veronica Nyahende amewataka wahitimu wa elimu ya juu nchini kutumia elimu waliyonayo kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa.

Alisema changamoto ya kurejesha mikopo  ni kubwa kwa upande wa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana kazi ama hawajajiajiri.
“Changamoto iliyopo ni wahitimu kushindwa kulipa mikopo hiyo kutokana na kuwa na kipato cha chini ama kukosa ajira.”

Alisema Bodi imeingia mkataba na kampuni zitakazokusanya mikopo kwa walionufaika na mikopo hiyo na kushindwa kuilipa .

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iko katika mchakato wa kuelimisha umma na watendaji wakuu Serikalini ili kuhakikisha wanawasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa mikopo hiyo.

Thursday, June 26, 2014

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA UTAWALA NA RASILIMALIWATU SERIKALINI


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Utumishi Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.


Washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue  (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.

Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutano mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungumkutano huo katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Bw. HAB Mkwizu .


Washiriki wa mkutano mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo  uliofanyika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.


Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. Solanus Nyimbi akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini baada ya ufunguzi wa mkutano  mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.

Sekretarieti ikichukua michango wakati wa mkutano  mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano  mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali katika ukumbi wa St. Gaspar  mjini Dodoma leo.

Monday, June 23, 2014

BALOZI SEFUE AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi, akiongea wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Meza kuu ikifuatilia burudani iliyotolewa na kikundi cha Machozi Theatre katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa taasisi mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipewa maelezo kuhusu maabara inayohamishika na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) Bw.Hiiti Sillo alipotembelea banda hilo kabla ya kufunga rasmi Maonyesho ya Wiki wa Utumishi wa Umma leo.


Kikundi cha Machozi Theartre kikitoa burudani.

Sunday, June 22, 2014

KAIMU KATIBU MKUU UTUMISHI BW.HAB MKWIZU ATEMBELEA MABANDA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dar es Salaa.Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw.Florence Temba.

Maafisa wa Banda la NIDA wakihudumia wateja kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akipewa maelezo na Maafisa wa NIDA  kuhusu Vitambulisho vya Taifa alipotembelea banda hilo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akipewa maelezo kuhusu ushirikiano uliopo kati ya  nchi za Afrika Mashariki na Afisa Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi.Robi Bwiru (wa pili kutoka kulia) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi.Vedastina Justinian (kulia).

Kaimu Katibu Mkuu Bw.HAB Mkwizu (kulia) akipewa maelezo na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Bi. Hellen Macha kuhusu masuala ya kiutumishi alipotembelea banda hilo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akipewa maelezo ya historia ya ndege za Serikali na Afisa Tawala wa Wakala wa Ndege za Serikali Bw. Francis N. Tumbo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Friday, June 20, 2014

KONGAMANO LA MIAKA 50 YA MUUNGANO LAFUNGWA RASMI

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu akifunga Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma kwa Niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

Mmoja wa wajumbe wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma akiwasilisha majumuisho ya maazimio ya kongamano hilo katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

MATUKIO MBALIMBALI YA KONGAMANO LA MIAKA 50 YA MUUNGANO KATIKA UTUMISHI WA UMMA ,KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO CHA MWALIMU NYERERE (JNICC) JIJINI DAR ES SALAAM

 
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu  Bw. Phillemon Luhanjo akitoa mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) leo.
Washiriki wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Bw.Phillemon Luhanjo wakati wa kongamano hilo.
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akiongoza Meza kuu wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma linaloendelea katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri  kazi Bw.Micky Kiliba,Katibu Mkuu Mstaafu Bi.Ryth Mollel na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Xavier Daudi.

Washiriki wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Bw.Phillemon Luhanjo wakati wa kongamano hilo.

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri  Kazi Bw.Micky Kiliba akichangia mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma lililofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

Mtendaji Mkuu Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt.Jabiri Kuwe Bakari akichangia mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma lililofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw.Mrisho Gambo akichangia mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma lililofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.