Tuesday, June 17, 2014

SERIKALI YAAGA WATAALAMU 9 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPAN

Mwakilishi Mwandamizi kutoka JAICA Bw. Yoichiro Kimataakiwatambulisha Wataalamu tisa wa kujitolea kutoka Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu. 

Mmoja kati ya Wataalamu wa kujtolea kutoka Japan Bi. Maiko Shimizu akieleza mafanikio ya kazi alizokua akifanya mkoani Dar es Salaam.

Mmoja kati ya Wataalamu wa kujtolea kutoka Japan Bw.Yoshiharu Kamata akieleza mafanikio ya kazi alizokua akifanya mkoani Mbeya.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kufanya kazi nchini.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akimkabidhi zawadi mmoja wa Wataalamu wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao hapa nchini Bi.Maiko Shimizu.

No comments:

Post a Comment