Monday, June 16, 2014

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2014 YAFUNGULIWA RASMI LEO

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Utawala Bora  Mhe.George  H. Mkuchika (Mb) akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mapema leo.Kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mapema leo.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora Mhe.George H. Mkuchika (Mb), Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Xavier Daudi na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Kuwe Bakari (wa kwanza kulia).

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (katikati) akifafanua jambo wakati mgeni rasmi Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Utawala Bora Mhe.George Mkuchika(Mb) (kushoto) alipotembelea mabanda ya Taasisi mbalimbali zinazoshiriki maonesho hayo. Kulia ni Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi.Ilham Mwinyi.



Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa katika banda la  Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakipewa maelezo kuhusu majukumu ya Ofisi ya Rais-Utumishi.

No comments:

Post a Comment