Friday, November 14, 2025
Thursday, November 13, 2025
Monday, November 10, 2025
KATIBU MKUU OFISI YA RAIS AWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUDUMISHA AMANI
Na Eric Amani, Dodoma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi,
ametoa wito kwa Watumishi wa Umma nchini kuendelea kudumisha amani, mshikamano na
uzalendo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya Taifa.
Akizungumza
jijini Dodoma leo tarehe 10 Novemba,
2025 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo
yanayofanyika kila siku ya Jumatatu,
Katibu Mkuu Mkomi amesema, Utumishi wa Umma una nafasi kubwa katika kulinda na kuimarisha
amani ya nchi kwa kutoa huduma bora, kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka
vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko katika jamii.
“Watumishi wa Umma ni kioo cha Serikali, hivyo mnapaswa kuwa mfano katika uadilifu, uvumilivu na
uzalendo,” alisema Katibu Mkuu Mkomi.
Bw.
Mkomi pia aliwakumbusha watumishi kuzingatia misingi ya utawala bora,
uwajibikaji, na matumizi sahihi ya rasilimali za umma, sambamba na kutumia
lugha na mienendo inayojenga taswira chanya ya Serikali.
Kwa upande wake mwewezeshaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa TEHEMA, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mussa Chiwelenje amewasisitiza Watumishi kutunza taarifa zao binafsi, za Ofisi na kutochezea miundombinu ya TEHAMA kwa usalama wa Taifa.
![]() |
| Mkurugenzi Kitengo cha Usalama wa Mtandao na TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mussa Chiwelenje akiwasilisha Mada ya usalama wa Mtandao kwenye Mafunzo ya Kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi ya Rais - UTUMISHI Novemba 10, 2025. |
![]() |
| Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Mussa Magufuli Novemba 10, 2025 akichangia Mada kwenye mafunzo ya Kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma. |















