Na Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 25.11.2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameisisitiza Mamlaka ya Serikali
Mtandao (e-GA) kuendelea kuunganisha mifumo ya Serikali
kwenye Mfumo wa Kuwezesha Mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana
taarifa (Government Enterprise Service Bus (GovESB) ili dhana ya kusomana kwa
mifumo hiyo ionekane kwa wananchi.
“Ninawasisitiza
Mifumo yote ambayo bado haijaunganishwa iunganishwe, dhana ya Mifumo kusomana
ionekana dhahiri kwa wananchi na kutoa mfano kuwa mwananchi anapoenda kupata
huduma akitoa namba yake ya NIDA taarifa zake zote za msingi zipatikane,” Mhe.
Kikwete amesisitiza.
Aidha,
Mhe. Kikwete ametoa wito kwa taasisi hiyo kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili
ya watumishi wake kujiendeleza ili kupata upeo mpana katika masuala ya
teknolojia ambayo yanakuwa kwa kasi.
Kwa upande wake Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray, ameomba ushirikiano toka kwa Watendaji wa Taasisi hiyo.
“Ili tuweze kufanya kazi vizuri
ni lazima tushirikiane, nitaendelea kuwa mwanafunzi wenu ili kazi ya Mamlaka
hii ifanyike vizuri kwa ufasaha.” Mhe. Qwaray ameongeza
Akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),
Mkurugenzi Mkuu wa eGA, Mhandisi Benedict Ndomba amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya umma
iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 yenye
jukumu la kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na
kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali
Mtandao kwa taasisi za umma.
Ameongeza kuwa e-GA inakusudia kutekeleza afua
mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi.
Mhe. Kikwete ameendelea na ziara
yake ya kikazi aliyoianza jana katika Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akiambatana na Naibu Waziri
wake Mhe. Regina Qwaray kwa lengo la kujitambulisha na kuboresha utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Viongozi pamoja watumishi wa Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi leo tarehe 25 Novemba, 2025 Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akitoa neno
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi hiyo Mhe.
Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)
wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi hao katika Ofisi hiyo leo tarehe 25 Novemba,2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa mbele) akifafanua jambo
wakati wa ziara yake katika Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) leo tarehe
25 Novemba,2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya eGA, Mhandisi
Benedict Ndomba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) leo tarehe 25 Novemba,
2025 baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwasili katika Ofisi hiyo katika ziara
yake ya kikazi jijini Dodoma
Menejimenti ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) akizungumza nao wakati alipowatembelea kufanya ziara yake ya kikazi
katika Ofisi hiyo leo tarehe 25 Novemba, 2025 jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani akisaini kitabu cha wageni
baada ya kuwasili Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwenye
ziara yake ya kikazi leo tarehe 25 November,2025 Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka wakati wa ziara yake ya kikazi
katika Ofisi ya Mamlaka
ya Serikali Mtandao (e-GA) leo tarehe 25 Novemba jijini Dodoma.
Menejimenti ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akizungumza nao wakati alipowatembelea kufanya
ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo tarehe 25 Novemba, 2025 jijini
Dodoma
Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka akijitambulisha kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Menejimenti ya Serikali Mtandao (e-GA) (hawapo pichani) baada ya Waziri huyo kuwasili katika Ofisi hiyo katika ziara yake ya kikazi leo 25 Novemba, jijini Dodoma
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Mamlaka Serikali Mtandao (e-GA) katika ziara ya kikazi leo tarehe 25, November,2025 Jijini Dodoma.
Menejimenti
na Watumisi wa Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wakiwa wanamsubiria Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete kuwasili katika Ofisi hiyo kwenye ziara yake ya kikazi tarehe25
Novemba, 2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) (hawapo pichani) leo tarehe 25.11.2025, jijini Dodoma alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ambapo ni mara ya kwanza kufika katika Ofisi hiyo tangu ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Mamlaka ya Serikali
Mtandao (e-GA) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo tarehe 25 Novemba, 2025 jijini Dodoma. kulia kwake
ni Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray na Kushoto kwake ni Katibu Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka.
Menejimenti
ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(hayupo pichani) akizungumza nao wakati alipowatembelea kufanya ziara yake ya
kikazi katika Ofisi hiyo leo tarehe 25 Novemba, 2025 jijini Dodoma







No comments:
Post a Comment